Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
Wachezaji wa Stellenbosch Football Club wamewasili Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya mashindano ya CAF Confederation Cup dhidi ya wenyeji wao Simba SC kutoka Tanzania. Mchezo huo wa kusisimua unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili, tarehe 20 Aprili 2025, katika dimba la kisasa la New Amaan Complex, Zanzibar, kufuatia kufungwa kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya ukarabati.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na timu ipo tayari kupambana kuhakikisha inasonga mbele hadi hatua ya fainali.
Ahmed amesisitiza kuwa Stellenbosch si timu ya kubezwa, kwani kufika kwao hatua ya nusu fainali ni ushahidi wa ubora wao, hivyo Simba italazimika kupambana vilivyo katika uwanja wa nyumbani. Ili mashabiki waweze kushuhudia pambano hilo la kihistoria, tiketi za kuingia uwanjani zimeanza kuuzwa rasmi. Tiketi hizo zinapatikana katika vituo mbalimbali vilivyoenea Dar es Salaam na Zanzibar, vikiwa ni sehemu maalum zilizoteuliwa na klabu kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wake.
Vituo Rasmi vya Kununua Tiketi
Ifuatayo ni orodha ya vituo rasmi vya kuuza tiketi kwa mechi kati ya Simba SC na Stellenbosch FC:
Dar es Salaam:
- Lampard Electronics – Simba HQ, Msimbazi
- Vunja Bei Shops – Maduka yote (Dar es Salaam)
- New Tech General Traders – Yeni Bar
- TTCL Shops – Dar es Salaam
- Juma Burrah – Msimbazi Center
- Halphani Hingaa – Oilcom Ubungo
- Mtemba Service Company – Temeke
- Jackson Kimambo – Ubungo Rombo
- Mkaluka Traders Ltd – Machinga Complex
- Khalfani Mohammed – Ilala Bungoni
- Karoshy Pamba Collection – Dar Live
- Fusion Sports Wear – Posta DSM
- Gwambina Lounge – Temeke Opp Duce
- Antonio Service Co. – Sinza & Kivukoni
- Gisela Shirima – Dahomey Street
- Tumpe Kamwela – Kigamboni
- Sovereign Co. – Kinondoni Makaburini
- Gitano Samwel – Mbagala Zakhem
- Robert Nyabululu – Ferry Kigamboni
- Nicovic Enterprises Ltd – Segerea Oilcom
- Sabana Business Center – Mbagala Maji Matitu
- Tawi la Simba – Kariume Unstoppable
Zanzibar:
- Amaan Stadium
- Mohamed Zahran Abdulla – Bandarini, Mkoani Pemba
- Shadrack Kimario – Kariakoo, Mchina Tambi
- Nuhu Jumanne Ally – Bububu Skuli
- Rashid Issa Juma – Fuoni (Mambo Sasa Nawasillisha)
- Lukuman Omar Khamis – Radio One, Daraja Bovu
- Harith – Amani
- Fahad – Kwerekwe
- Hamza – Melitano
- Suleiman – Kwerekwe Sokoni
- Hamid – Bububu
- Issa Yunus Issa – Fuoni Melinne
- Mwinyi Mwinyi Mwanakwerekwe – Car Wash
- TTCL Office – Kijangwani
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Stellenbosch Chawasili Zanzibar kwa Ajili ya Simba
- Ratiba ya Mechi za Leo 19/04/2025 Ligi Kuu NBC
- Msigwa Afunguka Kuhusu Ukarabati wa Uwanja wa Mkapa
- Polisi Tanzania Yajipanga Kulpa Kisasi Dhidi ya Mbeya City Babati
- Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba
- Wafungaji Bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
- Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Klabu bingwa UEFA Champions 2024/2025
- Simba SC Yasaini Mkataba Mnono wa Vifaa vya Michezo
Leave a Reply