Matokeo ya Darasa la Saba 2024 Mkoa wa Morogoro

Matokeo ya NECTA Kidato Cha Sita 2024 Haya Hapa

Matokeo ya Darasa la Saba 2024 Mkoa wa Morogoro | Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani ya darasa la saba mwaka 2024 huku ufaulu wa jumla ukiongezeka kwa asilimia 0.29 kulinganisha na mwaka 2023.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Said Mohamed aliyekuwa akitangaza matokeo hayo leo Oktoba 29, 2024 jijini Dar es Salaam amesema ufaulu wa jumla umeongezeka kutoka asilimia 80.58 iliyorekodiwa mwaka 2023 hadi asilimia 80.87 mwaka huu.

“Watahiniwa 974,229 wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B na C, Aidha takwimu zinaonesha kuwa ufaulu katika masomo yote sita yaliyotahiniwa umeendelea kuimarika,”amsesema Dk Mohamed/Matokeo ya Darasa la Saba 2024 Mkoa wa Morogoro.

Matokeo ya Darasa la Saba 2024 Mkoa wa Morogoro
Matokeo ya Darasa la Saba 2024 Mkoa wa Morogoro

Septemba 2024 jumla ya watahiniwa wa darasa la saba 1,204,899 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi sawa na asilimia 98 kati ya watahiniwa 1,230,774 waliosajiliwa kufanya mtihani huo.

Kati ya watahiniwa hao waliofaulu mtihani huo taarifa ya Necta inabainisha kuwa wavulana walikuwa 449,057 sawa na 46 na wasichana 525,172 sawana 54.

Aidha, Dk Mohamed amebainisha kuwa kuna uwiano sawa wa ufaulu kwa wasichana na wavulana katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka huu.

“Ubora wa ufaulu umeimarika kwa jinsi zote kwani kwa wasichana kuna ongezeko la asilimia 9 na kufikia asilimia 33 na wavulana kuna ongezeko la asilimia 8 na kufikia asilimia 39 kulinganisha na mwaka jana,” ameongeza Dk Mohamed.

Matokeo ya Darasa la Saba 2024 Mkoa wa Morogoro

Haya hapa matokeo ya Mkoa wa Morogoro:-

GAIRO

IFAKARA TC

KILOSA

MALINYI

MLIMBA

MOROGORO

MOROGORO MC

MVOMERO

ULANGA

Pendekezo la Mhariri:

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo