Kikosi cha Yanga Vs KMC Leo 29 September 2024 | Kikosi cha Yanga leo Dhidi ya KMC Ligi Kuu ya NBC
leo tarehe 29 Septemba 2024, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wanatarajia kushuka dimbani kuchuana na KMC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Mchezo huu unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa na mvuto wa kipekee kwa mashabiki wa soka nchini, ukizingatia historia ya timu hizi na mwenendo wa hivi karibuni katika ligi.
Yanga SC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya KMC. Katika mechi 12 zilizopita za Ligi Kuu walizokutana, Yanga imeshinda mara 9, KMC ikibeba ushindi mara moja tu, huku mechi mbili zikiishia kwa sare. Hii inaonyesha ni jinsi gani Yanga imekuwa na ubabe dhidi ya KMC, na historia hii inaweza kuipa Yanga motisha zaidi ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo.
Yanga imeanza msimu wa 2024/2025 kwa kishindo, ikiibuka na ushindi kwenye mechi zake zote mbili za awali za Ligi Kuu, ikifunga mabao matatu na bila kuruhusu bao lolote kufungwa.
Timu hii inajivunia safu kali ya ulinzi, ikiwa imefungwa bao moja tu katika mechi nane za mashindano mbalimbali tangu msimu uanze. Pia, safu yake ya ushambuliaji imekuwa hatari, ikifunga mabao 25 kwenye mechi hizo, jambo linalowafanya kuwa tishio kwa timu pinzani.
Katika mechi ya mwisho ya ligi, Yanga iliwalaza KenGold kwa bao 1-0, baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 2-0 ugenini. Mfululizo huu wa ushindi unaifanya Yanga kuingia kwenye mchezo huu dhidi ya KMC wakiwa na hali ya kujiamini. Kwa upande wa KMC, hali si shwari sana. Timu hii haijaonyesha uwezo wa kuvutia tangu msimu uanze, ikiwa imeshinda mechi moja tu, kutoka sare moja, na kupoteza mechi tatu. KMC imefunga mabao matatu tu huku ikiruhusu mabao saba kufungwa, jambo linaloashiria udhaifu katika safu yao ya ulinzi.
Hata hivyo, mchezaji wa kutegemewa kwa KMC, Redemptus Musa, amekuwa nguzo muhimu katika kikosi hicho, akifunga mabao mawili kati ya matatu ya timu yake msimu huu. Musa anatarajiwa kuwa mchezaji wa kuangaliwa zaidi kwenye mchezo huu, huku akihitajika kuonyesha makali yake dhidi ya safu ya ulinzi ya Yanga ambayo haijaruhusu mabao mengi msimu huu.
Kikosi cha Yanga Vs KMC Leo 29 September 2024
Kikosi cha Yanga dhidi ya KMC FC kinatarajiwa kutangazwa rasmi leo majira ya saa 2 usiku.
Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaotajwa na kocha wa Yanga kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kwa ajili ya mechi hii muhimu. Endelea kufuatilia chapisho ili ili kupata taarifa sahihi za kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa.
Hiki Apa kikosi Rasmi Cha yanga kilichotangazwa
Hiki apa kichosi ambacho sisi habariforum tunadhani kitaanzishwa na Miguel Gamond leo
- 39 Diarra
- 21 Yao
- 23 Boka
- 5 Job
- 4 Bacca
- 20 Mkude
- 9 Maxi
- 27 Mudathir
- 24 Muleke
- 10 Moloko
- 17 Chama
- 25 Pacome
Umuhimu wa Mchezo kwa Yanga na KMC
Kwa Yanga, ushindi kwenye mchezo huu utawapa nafasi nzuri ya kuendelea kuongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuimarisha nafasi yao ya kutetea ubingwa. Kwa KMC, ni nafasi ya kujitahidi kurekebisha hali yao ya msimu huu na kupata alama muhimu kwenye ligi, ingawa watakutana na changamoto kubwa kutoka kwa mabingwa watetezi.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply