Orodha ya Matajiri 10 Duniani 2024

Orodha ya Matajiri 10 Duniani 2024 | Majina ya Matajiri Duniani Agosti 2024 Forbes

Mwaka 2024 umeleta mabadiliko makubwa katika orodha ya matajiri duniani, ambapo majina makubwa katika sekta za teknolojia, bidhaa za anasa, na e-commerce yanaendelea kutawala. Hii ni orodha ya matajiri 10 duniani kwa mwaka 2024, ikionyesha jinsi vyanzo vyao vya utajiri vinavyowaweka katika nafasi hizi za juu.

Orodha ya Matajiri 10 Duniani 2024

Nafasi Jina Utajiri Umri Chanzo Cha Utajiri Uraia
1 Elon Musk $243.2 B 53 Tesla, SpaceX United States
2 Jeff Bezos $194.2 B 60 Amazon United States
3 Bernard Arnault & family $193.8 B 75 LVMH France
4 Mark Zuckerberg $180.5 B 40 Facebook United States
5 Larry Ellison $172.2 B 80 Oracle United States
6 Warren Buffett $143.0 B 93 Berkshire Hathaway United States
7 Larry Page $138.3 B 51 Google United States
8 Bill Gates $133.0 B 68 Microsoft United States
9 Sergey Brin $132.4 B 51 Google United States
10 Amancio Ortega $123.1 B 88 Zara Spain

1. Elon Musk

Elon Musk- Tajira wa kwanza duniani

  • Utajiri: $232.1 bilioni
  • Chanzo cha Utajiri: Tesla, SpaceX, X Corp.
  • Umri: Miaka 53
  • Uraia: Marekani

Elon Musk anaendelea kuongoza orodha ya matajiri duniani mwaka 2024 akiwa na utajiri wa dola bilioni 232.1. Musk ameimarisha nafasi yake kupitia mafanikio makubwa ya Tesla na SpaceX. Kampuni ya Tesla, inayozalisha magari ya umeme, imekuwa moja ya kampuni za thamani zaidi duniani, huku SpaceX ikivunja rekodi katika safari za anga za juu. Pia anamiliki X Corp., kampuni inayosimamia mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter).

2. Jeff Bezos

Jeff Bezos

  • Utajiri: $202 bilioni
  • Chanzo cha Utajiri: Amazon, Blue Origin
  • Umri: Miaka 60
  • Uraia: Marekani

Jeff Bezos, mwanzilishi wa Amazon, anakamata nafasi ya pili akiwa na utajiri wa dola bilioni 202. Amazon imeendelea kuongoza katika sekta ya e-commerce na huduma za wingu (cloud computing). Bezos pia ni mwanzilishi wa Blue Origin, kampuni inayojihusisha na safari za anga za juu kwa ajili ya utalii wa anga. Mbali na Amazon, Bezos anamiliki gazeti la The Washington Post na kampuni ya uwekezaji ya Bezos Expeditions.

3. Bernard Arnault na Familia

Bernard Arnault na Familia

  • Utajiri: $175.4 bilioni
  • Chanzo cha Utajiri: LVMH
  • Umri: Miaka 75
  • Uraia: Ufaransa

Bernard Arnault na familia yake wanashika nafasi ya tatu kwa utajiri wa dola bilioni 175.4. Arnault ni mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa LVMH, kampuni kubwa zaidi ya bidhaa za anasa duniani. LVMH inajumuisha bidhaa maarufu kama Louis Vuitton, Christian Dior, na Moët Hennessy. Kupitia uongozi wake, Arnault ameibadilisha LVMH kuwa kampuni ya kimataifa yenye ushawishi mkubwa katika sekta ya bidhaa za anasa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Orodha ya Matajiri Tanzania 2024
  2. Orodha ya Wasanii Matajiri Tanzania 2024
  3. Mishono Mipya Ya Vitambaa 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo