Matokeo ya Serengeti Boys vs Senegal Leo 02/06/2026
Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 almaarufu kama Serengeti Boys leo itashuka dimbani katika mchezo wa kuandika historia ambapo watachuana vikali na vijana wa Senegal katika mchezo wa fainali ya AFCON U-17 2026 utakaopigwa Rabat, Morocco.
Mchezo huu wa fainali utapigwa kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika Uwanja wa Prince Moulay Hassan jijini Rabat, Morocco. Serengeti Boys inaingia uwanjani ikiwa na nafasi ya kuandika historia kubwa kwa soka la Tanzania. Hii ni fainali muhimu kwa Tanzania, kwani Serengeti Boys imefika hatua hii kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo.
Matokeo ya Serengeti Boys vs Senegal Leo: Live Update
| Serengeti Boys | 1-1 FT | Senegal |
| Mikwaju ya Peniati | 2-4 PK | Mikwaju ya Peniati |

Taarifa Za Mchezo
| Mechi | Serengeti Boys vs Senegal |
| Mashindano | AFCON U-17 2026 |
| Hatua | Fainali |
| Tarehe | Juni 2, 2026 |
| Muda | Saa 4:00 usiku |
| Uwanja | Prince Moulay Hassan, Rabat, Morocco |
Kikosi cha Serengeti Boys Dhidi ya Senegal
Kikosi cha Serengeti Boys kitakachoanza dhidi ya Senegal kimetangazwa, huku kocha Elieneza Nsanganzelu akiwapa nafasi wachezaji 11 kuanza mchezo huu wa fainali.
Serengeti Boys XI
- 18. Haji Abdalah
- 14. Idrisa Kilendemeo
- 12. Elick Yusuph
- 3. Kassim Juma (C)
- 5. Hussein Mbegu
- 8. Issa Chole
- 17. Hamis Mihambo
- 15. Dismas Athanasi
- 11. Razaki Juma
- 10. Luqman Mbalasalu
- 19. Sadam Hamis
Wachezaji wa Akiba
- Rajabu Manyerezi
- Abraham Nassoro
- Hassan Mkindai
- Sultan Shamba
- George Mzungu
- Ismail Ukungilo
- Hasan Kizinga
Soann Shabani - Abdul Issa
- Hamisi Barua
Kocha: Elieneza Nsanganzelu
Serengeti Boys Inaingia Fainali Kwa Historia
Serengeti Boys imefika fainali ya AFCON U-17 kwa mara ya kwanza katika historia yake. Hatua hiyo tayari imeiweka Tanzania katika rekodi kubwa ya soka la vijana barani Afrika.
Timu hiyo ilitinga fainali baada ya kuiondoa Misri U-17 kwa mikwaju ya penalti 4-3, kufuatia sare tasa ndani ya dakika 90. Kabla ya hapo, Serengeti Boys pia iliitoa Algeria U-17 kwa mikwaju ya penalti katika hatua ya robo fainali.
Ushindi dhidi ya Senegal katika fainali hii utaipa Tanzania nafasi ya kutwaa taji kubwa la kwanza la soka la Afrika kupitia timu ya taifa.
Senegal Ilivyofika Fainali
Senegal nayo iliingia fainali baada ya kuiondoa Morocco kwa mikwaju ya penalti 7-6. Dakika 90 za nusu fainali hiyo zilimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Hii inaifanya fainali ya leo kuwa mchezo wa timu mbili zilizopitia presha kubwa katika hatua za mtoano. Kwa Serengeti Boys, nidhamu, umakini na utulivu vitakuwa muhimu katika kutafuta ushindi.
Umuhimu wa Matokeo Haya Kwa Tanzania
Matokeo ya Serengeti Boys vs Senegal leo yana uzito mkubwa kwa sababu Tanzania haijawahi kutwaa taji la AFCON kupitia timu ya taifa. Serengeti Boys ina nafasi ya kuwa timu ya kwanza ya taifa ya Tanzania kubeba kombe la Afrika.
Hata kabla ya fainali hii, Serengeti Boys tayari imefanikiwa kufuzu Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17 litakalofanyika Qatar kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 13, 2026.
Mafanikio hayo tayari ni hatua kubwa kwa soka la vijana nchini, lakini ushindi wa leo unaweza kuifanya safari hii kuwa moja ya kurasa muhimu zaidi katika historia ya soka la Tanzania.
Kocha Elieneza Aizungumzia Fainali
Kocha Elieneza Nsanganzelu amesema wachezaji wake wako tayari kwa mchezo dhidi ya Senegal.
“Tunamshukuru Mungu vijana wote wako salama na wanapumzika vizuri. Watanzania waendelee kuiamini timu yao. Maandalizi yanaendelea vizuri. Tunashukuru serikali imeonyesha kuwa iko nyuma ya timu,” alisema Nsanganzelu.
Akizungumzia mpinzani wao, kocha huyo alisema: “Senegal ni timu inayopenda kutumia miili. Staili yao ya uchezaji, wanapokuwa na mpira wanataka kufika golini kwa haraka. Hamna fainali ambayo huwa rahisi, utakuwa mchezo mgumu na kwa hatua tuliyofika tutaenda tukichukulia mechi ni ngumu na sisi tuko tayari kucheza na Senegal.”
Tuzo na Ahadi Kwa Serengeti Boys
Serengeti Boys tayari ina uhakika wa kupata Sh500 milioni kutokana na ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan kama pongezi kwa kufika fainali ya AFCON U-17 2026.
Fedha hizo zitatolewa iwe timu itashinda au kupoteza mchezo wa fainali. Ikiwa Serengeti Boys itatwaa ubingwa, kila mchezaji pia ameahidiwa kiwanja mkoani Morogoro.
Kwa upande wa CAF, bingwa wa mashindano haya atapata Dola 125,000, huku mshindi wa pili akipata Dola 90,000.
Matokeo Yataweka Historia Mpya
Macho ya Watanzania leo yako Rabat, Morocco, ambako Serengeti Boys inakutana na Senegal katika fainali ya AFCON U-17 2026. Mchezo huu si wa kutafuta kombe pekee, bali pia ni nafasi ya kuthibitisha maendeleo ya soka la vijana nchini.
Matokeo ya Serengeti Boys vs Senegal leo yataamua kama Tanzania itaandika historia ya kutwaa taji lake la kwanza kubwa la Afrika kupitia timu ya taifa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- PSG Mabingwa Tena UEFA Champions League Baada ya Ushindi wa Penalti Dhidi ya Arsenal
- Liverpool Yaachana na Arne Slot, Iraola Apewa Nafasi Kubwa Kumrithi
- Ratiba Ligi Kuu Bara 2026 Yawagawa Wadau Baada ya Msimu Kusogezwa Hadi Juni 30
- Ratiba ya Kombe la Dunia 2026: Mechi Zote, Tarehe, Viwanja na Makundi
- Yanga Yaiingilia Azam Dili la Winga Mkongo Henoc Molia
```






Leave a Reply