Msimamo wa Ligi Kuu Ya NBC 10 Mei 2026 Baada ya Mechi za Leo
Mbio za kumsaka bingwa wa ligi kuu msimu wa 2025/2026 zinaendelea ambapo mashabiki watashuhudia michezo mitatu itakayochezwa katika viwanja tofauti. Mechi hizo zina umuhimu mkubwa kwenye msimamo, zikihusisha timu zinazowania ubingwa, zile zinazopigania nafasi za kati, pamoja na timu zilizo kwenye presha ya kukwepa kushuka daraja.
Kwa mujibu wa msimamo wa sasa, Young Africans bado inaongoza ligi ikiwa na pointi 54 baada ya michezo 22, huku Simba ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 46 baada ya kucheza mechi 21. Azam ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 43 baada ya michezo 22.
Taarifa: Msimamo huu unaonyesha hali ya ligi kabla ya mechi za leo kukamilika. Baada ya michezo ya leo kumalizika, ukurasa huu utasasishwa kwa matokeo rasmi, pointi mpya na mabadiliko yote muhimu kwenye jedwali.
Mechi za Ligi Kuu Ya NBC Leo 10 Mei 2026
Leo kutakuwa na michezo mitatu ya Ligi Kuu Ya NBC, huku macho mengi yakielekezwa kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.
| Muda | Mechi | Uwanja |
|---|---|---|
| Saa 8:00 mchana | KMC 2-3 Fountain Gate | KMC Complex |
| Saa 10:00 jioni | Pamba Jiji 0-0 Dodoma Jiji | CCM Kirumba, Mwanza |
| Saa 1:00 usiku | Simba 4-0 Tanzania Prisons | Mechi Inaendelea | KMC Complex, Dar es Salaam |
Msimamo wa Ligi Kuu Ya NBC Kabla ya Mechi za Leo 10/05/2026
| Nafasi | Timu | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pointi |
| 1 | Young Africans | 22 | 16 | 6 | 0 | 50 | 5 | 45 | 54 |
| 2 | Simba | 22 | 14 | 7 | 1 | 39 | 9 | 30 | 49 |
| 3 | Azam FC | 22 | 11 | 10 | 1 | 31 | 9 | 22 | 43 |
| 4 | Singida Black Stars | 22 | 10 | 5 | 7 | 29 | 23 | 6 | 35 |
| 5 | JKT Tanzania | 22 | 9 | 8 | 5 | 22 | 21 | 1 | 35 |
| 6 | TRA United | 22 | 9 | 6 | 7 | 27 | 20 | 7 | 33 |
| 7 | Pamba | 22 | 7 | 9 | 6 | 22 | 22 | 0 | 30 |
| 8 | Dodoma Jiji FC | 22 | 7 | 8 | 7 | 19 | 21 | -2 | 29 |
| 9 | Mashujaa FC | 22 | 5 | 11 | 6 | 11 | 17 | -6 | 26 |
| 10 | Namungo FC | 22 | 5 | 9 | 8 | 17 | 23 | -6 | 24 |
| 11 | Mtibwa Sugar | 22 | 5 | 8 | 9 | 16 | 29 | -13 | 23 |
| 12 | Fountain Gate | 22 | 6 | 5 | 11 | 16 | 32 | -16 | 23 |
| 13 | Coastal Union | 22 | 5 | 7 | 10 | 20 | 29 | -9 | 22 |
| 14 | Mbeya City | 22 | 5 | 6 | 11 | 18 | 32 | -14 | 21 |
| 15 | Tanzania Prisons | 22 | 3 | 5 | 14 | 11 | 32 | -21 | 14 |
| 16 | KMC | 22 | 2 | 4 | 16 | 10 | 34 | -24 | 10 |
Simba Yaitafuta Tanzania Prisons Kuendelea Kuipa Presha Yanga
Simba inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 46, nyuma ya Young Africans ambayo inaongoza msimamo. Wekundu wa Msimbazi wanahitaji ushindi ili kuendelea kupunguza presha kwenye mbio za ubingwa na kuzuia pengo la pointi dhidi ya vinara kuendelea kuwa kubwa.
Simba inatoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, matokeo yaliyoiweka kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kuwania ubingwa. Hata hivyo, mchezo dhidi ya Tanzania Prisons unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia ya timu hizo zinapokutana.
Katika rekodi za ligi, Simba na Tanzania Prisons zimekutana mara 19, ambapo Simba imeshinda mechi 12, Tanzania Prisons imeshinda mechi nne, huku michezo mitatu ikiisha kwa sare.
Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola, alisema mchezo huo hautakuwa rahisi licha ya tofauti ya nafasi kwenye msimamo.
“Siku zote hakuna mechi rahisi kati yetu Simba na Prisons, mechi hii itakuwa ngumu, tumejipanga kukabiliana na ugumu huo, tumejiandaa vizuri kutafuta ushindi ili kuendelea kuutafuta ubingwa msimu huu,” alisema Matola.
Tanzania Prisons ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 21. Timu hiyo ipo kwenye presha kubwa ya kujinasua kwenye eneo la hatari, lakini hata ikishinda leo bado itaendelea kusalia nafasi ya 15 kutokana na tofauti ya pointi kati yake na Mbeya City iliyopo nafasi ya 14 kwa pointi 21.
Kocha wa Tanzania Prisons, Shadrack Nsajigwa, alisema timu yake haijakata tamaa licha ya kuwa kwenye hali ngumu.
“Nikweli hatupo kwenye nafasi nzuri lakini hatuna nafasi ya kukata tamaa, lolote linaweza kutokea, haitakuwa mechi rahisi kwetu dhidi ya Simba lakini tumejiandaa kukabiliana nao, tunataka kutafuta pointi yoyote kesho,” alisema Nsajigwa.

KMC Yaingia Kwenye Mechi Ngumu Dhidi ya Fountain Gate
Mchezo wa mapema utakuwa kati ya KMC na Fountain Gate. KMC ipo mkiani mwa msimamo ikiwa na pointi tisa baada ya mechi 21, hali inayoiweka kwenye presha kubwa ya kushuka daraja.
KMC imepoteza mechi nne kati ya tano za mwisho na kupata sare moja pekee. Matokeo mabaya katika michezo miwili ijayo yanaweza kuiweka kwenye nafasi ngumu zaidi kuelekea mwisho wa msimu.
Fountain Gate ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 22 baada ya michezo 21. Ingawa haipo salama kabisa, ushindi dhidi ya KMC unaweza kuisaidia kuongeza pengo dhidi ya timu zilizo chini ya msimamo.
Pamba Jiji na Dodoma Jiji Kupambania Pointi Tatu Muhimu
Pamba Jiji itakuwa nyumbani dhidi ya Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Huu ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili kwa sababu tofauti yao ni pointi moja pekee.
Pamba Jiji ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi 29 baada ya michezo 21, wakati Dodoma Jiji ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 28. Ushindi kwa upande wowote unaweza kubadilisha nafasi zao kwenye msimamo na kuziweka kwenye mazingira bora zaidi kuelekea michezo inayofuata.
Pamba Jiji imeshinda mechi moja tu kati ya tano za mwisho, ikipoteza tatu na kupata sare moja. Dodoma Jiji, kwa upande wake, imeshinda mechi mbili kati ya tano za mwisho, ikipoteza mbili na kupata sare moja.
Mabadiliko Yanayoweza Kutokea Baada ya Mechi za Leo
Mechi za leo zinaweza kuleta mabadiliko kwenye maeneo kadhaa ya msimamo.
Simba ikishinda dhidi ya Tanzania Prisons, itafikisha pointi 49 na kuendelea kuipa presha Young Africans kileleni. Pamba Jiji ikishinda dhidi ya Dodoma Jiji, itafikisha pointi 32 na kuimarisha nafasi yake ya saba. Dodoma Jiji ikishinda, itafikisha pointi 31 na kuipiku Pamba Jiji.
Kwa upande wa chini ya msimamo, Fountain Gate ikishinda dhidi ya KMC itafikisha pointi 25 na kupunguza presha ya eneo la kushuka daraja. KMC, ambayo tayari ipo nafasi ya mwisho, inahitaji matokeo chanya ili kuendelea kuwa na matumaini ya kujinasua.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026
- Kikosi cha Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026
- Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026 Saa Ngapi?
- Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/05/2026
- Yanga Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mrithi wa Pedro
- Mambo 6 Yaliyosababisha Pedro Kufungashiwa Vilago Yanga
- Harry Kane Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Ligi ya Mabingwa Ulaya
- Rasmi: Simba SC Yahamishia Michezo ya Nyumbani Uwanja wa KMC






Leave a Reply