Kikosi cha Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026

Kikosi cha Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo watakuwa dimbani kusaka pointi tatu nyingine watakapokabiliana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Mchezo huo unawakutanisha Simba iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 46 dhidi ya Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 14. Simba inaendelea na hesabu za kuutafuta ubingwa, huku Prisons ikipambana kuondoka kwenye presha ya mkia wa msimamo.

Kikosi cha Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026

Hiki Apa Kikosi cha Simba Kilichotangazwa

  • 39 KASSALI
  • 15 DUCHU
  • 5 MLIGO
  • 4 VEDASTUS
  • 25 TOURE
  • 21 KAGOMA
  • 7 GUEYE
  • 8 KANTE
  • 40 MWALIMU
  • 17 CHAMA [C]
  • 18 MORICE

Kwenye Benchi: ABEL, CHASAMBI, KIBABAGE, SEMFUKO, DIRA, NED, BARAKA, INNO, MPANZU, BASHIR.

Simba inaingia kwenye mchezo huu ikitoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania. Hata hivyo, Wekundu hao wamelazimika kuhamia KMC Complex baada ya awali kutumia Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Kwa upande wa mbio za ubingwa, Simba inaendelea kuifukuzia Yanga ambayo ni bingwa mtetezi na kinara wa ligi. Kabla ya Yanga kucheza dhidi ya Coastal Union, tofauti kati ya timu hizo ilikuwa pointi tano, jambo linaloifanya Simba kuhitaji ushindi ili kuendelea kuweka presha juu ya mpinzani wake.

Historia ya kukutana kwa Simba na Tanzania Prisons inaipa Simba rekodi bora zaidi. Timu hizo zimekutana mara 19 kwenye ligi, Simba ikishinda mechi 12, Tanzania Prisons ikishinda nne, huku mechi tatu zikimalizika kwa sare.

Simba pia imekuwa na mwendo mzuri katika mechi tano za mwisho, ikishinda tatu dhidi ya JKT Tanzania, Namungo na Fountain Gate, pamoja na sare mbili dhidi ya Yanga na TRA United. Tanzania Prisons, kwa upande wake, imepoteza mechi nne kati ya tano za mwisho dhidi ya Mbeya City, TRA United, Yanga na Singida Black Stars, huku ikipata sare moja dhidi ya KMC.

Ushindi wa mwisho wa Prisons ulikuwa Februari 14, 2026, ilipoifunga Namungo mabao 3-2 nyumbani. Tangu Shadrack Nsajigwa apewe majukumu ya kuinoa timu hiyo, bado hajapata ushindi.

Matola Aonya Kuhusu Ugumu wa Mechi

Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema wanatarajia mchezo mgumu licha ya Prisons kuwa katika nafasi ya chini kwenye msimamo. Kwa mujibu wake, historia ya timu hizo inapokutana ndiyo inayoufanya mchezo huo kuwa na uzito wake.

“Siku zote hakuna mechi rahisi kati yetu Simba na Prisons, mechi hii itakuwa ngumu, tumejipanga kukabiliana na ugumu huo, tumejiandaa vizuri kutafuta ushindi ili kuendelea kuutafuta ubingwa msimu huu,” alisema Matola.

Simba itawakosa wachezaji wawili katika mchezo huo. Nahodha Shomari Kapombe ni majeruhi, huku winga Anicet Oura, licha ya kurejea mazoezini, akitajwa kutokuwa na uwezekano mkubwa wa kucheza leo.

Kwa Tanzania Prisons, mchezo huu unabeba uzito mkubwa kutokana na nafasi yake kwenye msimamo. Hata kama itashinda, bado itaendelea kubaki nafasi ya 15 kutokana na tofauti ya pointi dhidi ya Mbeya City, iliyo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 21.

Kocha wa Prisons, Shadrack Nsajigwa, amekiri kuwa timu yake ipo katika hali ngumu, lakini amesema hawana nafasi ya kukata tamaa.

“Nikweli hatupo kwenye nafasi nzuri lakini hatuna nafasi ya kukata tamaa, lolote linaweza kutokea, haitakuwa mechi rahisi kwetu dhidi ya Simba lakini tumejiandaa kukabiliana nao, tunataka kutafuta pointi yoyote kesho (leo),” alisema Nsajigwa.

Umuhimu wa Mchezo kwa Pande Zote Mbili

Kwa Simba, mchezo huu ni nafasi ya kuendelea kukusanya pointi muhimu katika mbio za ubingwa. Ushindi utaifanya iendelee kuweka presha kwa Yanga na kuongeza nguvu kwenye hesabu zake za msimu.

Kwa Tanzania Prisons, kila pointi ina thamani kubwa katika mapambano ya kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja. Ingawa rekodi za karibuni haziipi nguvu kubwa, kauli ya Nsajigwa inaonyesha timu hiyo inaingia uwanjani ikiwa na lengo la kupambana kupata matokeo.

Mchezo wa leo kati ya Simba na Tanzania Prisons unatarajiwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili, kila moja ikiwa na malengo tofauti kwenye msimamo. Simba inahitaji ushindi ili kuendelea kuutafuta ubingwa, wakati Prisons ikitafuta pointi za kupunguza presha ya mkia.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026
  2. Kikosi cha Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026
  3. Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026 Saa Ngapi?
  4. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/05/2026
  5. Yanga Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mrithi wa Pedro
  6. Mambo 6 Yaliyosababisha Pedro Kufungashiwa Vilago Yanga
  7. Harry Kane Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Ligi ya Mabingwa Ulaya
  8. Rasmi: Simba SC Yahamishia Michezo ya Nyumbani Uwanja wa KMC
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo