Matokeo ya Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026

Matokeo ya Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026

Yanga inaingia kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ikiwa na jukumu la kutafuta ushindi ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara msimu huu. Mchezo huu unakuja wakati Yanga ikiwa imeachwa pointi tano na Simba, jambo linaloongeza umuhimu wa matokeo kwa upande wa mabingwa hao watetezi.

Kaimu kocha mkuu wa Yanga, Abdihamid Moalin, amesema timu yake imejiandaa kwa mchezo huo kwa kuzingatia falsafa ya kumiliki mpira na kudumisha viwango bora vya wachezaji.

“Falsafa yangu ni kuhakikisha timu inatawala mpira na kuumiliki, kuhakikisha tunamentain viwango bora vya wachezaji, hivyo tupo tayari kwa ajili ya mechi hiyo,” amesema Moalin.

Moalin amechukua mikoba ya Pedro Goncalves, aliyefutwa kazi baada ya kuisaidia Yanga kushinda bao 1-0 dhidi ya KMC. Katika mchezo wa leo, Yanga itahitaji kuendeleza mwendelezo wake mzuri kwenye ligi, ikiwa tayari imeshinda mechi 15 na kutoka sare sita katika michezo 21.

Kwa takwimu za msimu huu kabla ya mchezo huu, Yanga ina pointi 51, imefunga mabao 47 na kuruhusu mabao matano pekee. Coastal Union, ambayo ipo nafasi ya 12, imecheza mechi 21, ikishinda tano, kutoka sare saba na kufungwa tisa. Timu hiyo imefunga mabao 20, imeruhusu 26 na ina pointi 22.

Kipa wa Yanga, Abdultwalib Mshery, amesema wachezaji wamepokea maelekezo ya benchi la ufundi na wapo tayari kwa mchezo huo.

“Kila kocha ana mbinu zake ambazo tutatakiwa kuzifuata, lakini Kocha Moalin tulikuwepo naye, amerejea kwa mara nyingine, lakini kuhusu mechi dhidi ya Coastal, tumejipanga kwa ushindi,” amesema Mshery.

Kwa upande wa Coastal Union, kocha Fikiri Elias amesema anatarajia mchezo mgumu na wa ushindani, huku akieleza kuwa timu yake imetumia muda uliopatikana kuboresha maeneo muhimu.

“Natarajia mechi itakuwa ngumu na ya ushindani, tayari tumepata muda wa siku mbili kuboresha na kuimarisha baadhi ya maeneo ili kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Elias.

Kikosi cha Yanga Kilichotangazwa

Yanga imetangaza kikosi kitakachoanza mchezo dhidi ya Coastal Union, kikiongozwa na kipa Diarra. Wachezaji wengine waliotajwa ni Yao, Boka, Mwamnyeto, Bacca, Abuya, Maxi, Sheikhan, Dube, Okello na Pacome.

Kwenye benchi, Yanga imemtaja Masalanga, Abubakar, Kibwana, Assink, Abdulnasir, Damaro, Faridi, SureBoy, Mwanengo na Depu.

Katika upande wa safu ya ushambuliaji, Prince Dube ndiye kinara wa mabao wa Yanga akiwa na mabao tisa. Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua wanafuata, kila mmoja akiwa na mabao saba.

Kwa upande wa Coastal Union, Maabad Maulid na Shiza Kichuya kila mmoja ana mabao manne, huku Cleophace Mkandala akiwa na mabao matatu.

Matokeo ya Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026

Fuatilia Matokeo ya Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026

Yanga ScVSCoastal Union

🏆 #nbcpremierleague
🆚 Coastal Union
🗓️ 09 May 2026
🏟️ KMC Complex
⏱️ 12:15 Jioni

Umuhimu wa Mchezo kwa Yanga na Coastal Union

Mchezo huu una uzito mkubwa kwa Yanga kutokana na nafasi yake kwenye mbio za ubingwa. Timu hiyo inahitaji ushindi ili kuendelea kupunguza pengo la pointi na kuimarisha nafasi yake katika msimamo wa ligi.

Coastal Union nayo inaingia uwanjani ikiwa na hitaji la kufanya vizuri baada ya kukusanya pointi 22 katika mechi 21. Kwa mujibu wa kocha wake, maandalizi yamejikita katika kuboresha maeneo yaliyohitaji marekebisho kabla ya kukutana na Yanga.

Kwa takwimu zilizopo kabla ya mchezo, Yanga inaonekana kuwa na uimara mkubwa kwenye safu ya ulinzi na ushambuliaji, huku Coastal Union ikihitaji nidhamu kubwa ya mchezo ili kupata matokeo chanya.

Matokeo ya Yanga vs Coastal Union leo yanatarajiwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili. Yanga inahitaji ushindi ili kuendelea kubaki kwenye mbio za kutetea ubingwa, wakati Coastal Union itahitaji kupambana kupata matokeo yatakayoiweka katika nafasi nzuri zaidi kwenye msimamo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026
  2. Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026 Saa Ngapi?
  3. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/05/2026
  4. Yanga Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mrithi wa Pedro
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo