Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu 2024 | Njia rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA kwa Simu.
Namba ya NIDA (National Identification Number) ni utambulisho muhimu kwa kila Mtanzania. Namba hii hutumika katika kukamilisha huduma mbalimbali muhimu nchini ikiwemo usajili wa laini za simu, Usajili mashuleni, Kujaza fomu za mikopo n.k. Apo awali wakati NIDA inaanzishwa kulikuwa na changamoto kubwa ya kupata namba ya NIDA lakini kuanzia mwaka 2024, kupata namba hii muhimu kumekuwa rahisi zaidi, kwani sasa inawezekana kuipata moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi.
Kupata namba ya NIDA kwa simu ni hatua nzuri na yenye urahisi mkubwa katika kuhakikisha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinapatikana kwa urahisi. Ni njia rahisi na ya haraka ambayo inawawezesha watu wengi zaidi kupata huduma muhimu bila kulazimika kusafiri umbali mrefu au kusubiri kwa muda mrefu kwenye foleni katika ofisi ya NIDA.
Tumeandaa Makala haya kukupitisha katika njia rahisi na za haraka za kupata namba ya NIDA kwa Simu 2024. Tutakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kutumia njia mbalimbali ikiwemo USSD, SMS, na hata kupiga simu kwenye huduma kwa wateja. Pia, tutaelezea mahitaji muhimu unayopaswa kuwa nayo kabla ya kuanza mchakato huu.
Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu 2024
Kupata namba ya NIDA kumekuwa rahisi zaidi kuliko hapo awali. Sasa mtu yeyote anaweza kupata namba ya NIDA kwa urahisi na haraka kupitia simu ya mkononi, bila kujali mahali alipo au aina ya simu anayotumia. Hadi hivi sasa kuna njia kuu mbili za kupata namba ya NIDA kwa kutumia simu ya mkononi. Njia hizi ni kama zifuatazo;
- Kupitia USSD: Huu ni mfumo unaokuwezesha kuingiliana na kompyuta ya NIDA kwa kutumia misimbo maalumu. Ni njia rahisi na ya haraka ambayo haihitaji muunganisho wa intaneti.
- Kupitia SMS: Njia hii inahusisha kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba maalum ya NIDA. Kama ilivyo kwa USSD, njia hii pia haihitaji muunganisho wa intaneti.
Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu Kupitia USSSD
USSD (Unstructured Supplementary Service Data) ni njia rahisi na ya haraka ya kupata namba ya NIDA bila kuhitaji muunganisho wa intaneti. Fuata hatua hizi rahisi:
- Piga *152*00# kwenye simu yako ya mkononi.
- Chagua namba 3 (Ajira na Utambuzi).
- Chagua namba 2 (NIDA).
- Ingiza majina yako matatu (3) uliyojisajili (Mfano: Dan John Sele).
- Ingiza namba ya simu uliyojaza kwenye fomu ya maombi (Mfano: 0XXXXXXX).
- Kubali ombi lako.
- Utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye namba yako ya NIDA.
Huduma hii kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa Airtel na Vodacom.
Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu Kupitia SMS
Njia nyingine rahisi ya kupata namba yako ya NIDA ni kupitia SMS. Fuata hatua hizi:
- Andika ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye majina yako matatu (3) uliyojisajili (Mfano: Dan John Sele).
- Tuma SMS hiyo kwenda namba 15096.
- Utapokea ujumbe wa kujibu wenye namba yako ya NIDA. Huduma hii ni bure na inapatikana kwa mitandao yoteya simu nchini Tanzania.
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Jinsi Ya Kuangalia Deni La Gari 2024 (TMS Traffic Check)
- Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
- Jinsi Ya Kuangalia Namba Ya Simu Airtel, Vodacom, TTCL, Tigo & Halotel
- Jinsi Ya Kuangalia Usajili Wa Namba ya Simu
- Jinsi Ya Kuangalia Salio La Vifurushi Airtel 2024
- Jinsi Ya Kujiunga Na Vifurushi Vya Startimes 2024
Hiyo njia ya sms namba mbili haileti nida ukichagua inaleta postkod