Nauli ya Basi Dar Es Salaam kwenda Morogoro 2024

Nauli ya Basi Dar Es Salaam kwenda Morogoro 2024 | LATRA Nauli ya Basi Dar Es Salaam to Morogoro 2024

Safari ya basi kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ni moja kati ya safari zenye idadi kubwa ya wasafiri kutokana na shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi zinazoendelea baina ya mikoa hii miwili muhimu. Safari hii, ambayo huchukua takribani masaa matatu hadi manne kutegemeana na aina ya basi na hali ya barabara, inahudumiwa na makampuni mbalimbali ya usafiri yanayotoa huduma za usafiri wa basi.

Miongoni mwa makampuni maarufu yanayo toa huduma ya kusafirisha abiria kutoka dar es salaam kwenda Morogoro ni BM, Abbood Bus, New force, shabibi line, Kimbinyiko n.k. Makampuni haya yamekua yakitoza nauli kulingana na viwango vilivyopangwa na LATRA (Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini).

Kama wewe ni miongoni mwa maelfu ya wasafiri wanaotarajia kusafiri kutoka jiji la kibiashara Dar es Salaam hadi kitovu cha kilimo Morogoro mwaka huu wa 2024, na ungependa kujua nauli za mabasi, basi umefika mahali sahihi. Tumekusanya taarifa kamili kuhusu nauli za mabasi kwa mwaka 2024 kama zilivyopangwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).

Nauli ya Basi Dar Es Salaam kwenda Morogoro 2024

Hadi hii leo May 2024, nauli za mabasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro zimewekwa kama ifuatavyo kulingana na aina ya basi na mamlaka husika (LATRA):

Aina ya Basi Nauli (Tsh) Umbali (km)
Basi la kawaida (Ordinary) 9,000 192
Basi la kifahari (Luxury) 13,000 192

Nauli ya Basi Dar Es Salaam kwenda Morogoro 2024

Tafadhali kumbuka kwamba nauli hizi zinaweza kubadilika kidogo kulingana na kampuni ya basi unayochagua kusafiri nayo. Baadhi ya kampuni huenda zikatoza kiasi kidogo zaidi au kidogo chini ya bei hizi elekezi za kawaida.

Ili kupata taarifa ya uhakika zaidi kuhusu nauli za mabasi, tunashauri uwasiliane moja kwa moja na kampuni ya basi unayotaka kusafiri nayo au kutembelea tovuti yao rasmi. Unaweza kununua tiketi yako moja kwa moja kwenye vituo vya mabasi au kupitia tovuti za kampuni za mabasi husika. Inashauriwa kununua tiketi mapema, hasa wakati wa misimu ya kusafiri yenye wasafiri wengi, ili kuepuka usumbufu wowote.

Angalia: Vigezo & Sifa za Kujiunga JKT Mujibu Wa Sheria 2024

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo