Yanga vs TRA United Leo 27/06/2026 Saa Ngapi?

Yanga vs TRA United Leo 27/06/2026 Saa Ngapi?

Mechi ya Yanga vs TRA United leo itachezwa saa 10:00 jioni katika Uwanja wa KMC Complex. Mechi hii ni sehemu ya raundi ya 29 ya NBC Premier League.

Kwa mujibu wa ratiba mechi hii ni miongoni mwa mechi nane ambazo zitatimua vumbi katika vwanja tofauti nchini, mechi zote nane za ligi leo zitachezwa saa 10:00 jioni na zitakuwa mubashara kupitia AzamTV. Mbali na Yanga dhidi ya TRA United, mchezo mwingine mkubwa siku hii ni Simba SC dhidi ya Singida BS katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo.

Muhtasari wa Yanga vs TRA United Leo

KipengeleTaarifa
MechiYanga vs TRA United
MashindanoNBC Premier League
RaundiRaundi ya 29
Tarehe27 Juni 2026
Muda10:00 jioni
UwanjaKMC Complex
MatangazoAzamTV

Yanga vs TRA United Leo 27/06/2026 Saa Ngapi?

TRA United Yaenda Kupambana kwa Malengo Yake

Beki wa TRA United, Nasri Kombo, amesema timu yao haiendi kwenye mchezo dhidi ya Yanga kwa lengo la kuisaidia timu nyingine, bali inapambana kwa manufaa yake.

TRA United inaingia kwenye mchezo huu ikiwa imetoka kupata sare mfululizo dhidi ya Coastal Union na Namungo. Mara ya mwisho timu hiyo kupata ushindi ilikuwa Juni 12, 2026, ilipoifunga KMC.

Kwa sasa TRA United inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi. Imecheza mechi 28, ikishinda 11, kutoka sare tisa na kupoteza nane, ikiwa na jumla ya pointi 42.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nasri alisema hatua za mwisho za ligi zinahitaji kila timu kupambana kwa malengo yake.

“Tunakwenda kutafuta ushindi kwa manufaa yetu sisi na si kwa ajili ya kuisaidia timu nyingine. Kwenye ligi kila timu inapambana kwa malengo yake.”

Nasri: Yanga Ni Timu Nzuri, Lakini TRA Haitajiona Dhaifu

Nasri amesema TRA United inatambua ukubwa wa mchezo na ubora wa Yanga, lakini hilo halibadilishi malengo yao ya kwenda kushindana.

Alikumbushia mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Arusha, ambako TRA United ilitoka sare na Yanga. Kwa mujibu wake, matokeo hayo yanawapa imani ya kwenda kupambana tena.

“Tunaifahamu Yanga ni timu nzuri, lakini tulipopata nao sare Arusha tuliona inawezekana kupambana nao. Tunajua safari hii itakuwa mechi ngumu zaidi kwa sababu wanaweza kuingia wakitaka kulipa kisasi.”

Amesema katika kipindi hiki cha mwisho wa ligi, kila pointi ina uzito mkubwa na hakuna timu inayocheza kwa mazoea.

“Katika kipindi hiki hakuna timu inayocheza kwa mazoea na kila pointi imekuwa na uzito wake. Hivyo, TRA United itaingia uwanjani ikiwa na lengo la kupambana hadi mwisho ili kupata matokeo tunayoyahitaji,” amesema Nasri.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Ligi Kuu NBC Leo Juni 27, 2026: Yanga, Simba na Vita ya Kushuka Daraja
  2. Azam FC Yakaribia Kukamilisha Usajili wa Nyota Wawili Kutoka DR Congo
  3. Mtibwa Sugar vs Simba SC Leo 24/06/2026 Saa Ngapi? Ratiba, TV na Umuhimu wa Mechi
  4. Yanga vs Azam Leo 24/06/2026 Saa Ngapi? Ratiba, TV na Umuhimu wa Mechi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo