Matokeo ya Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026
Kikosi cha Simba leo kinashuka dimbani kuwakabili Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na uzito mkubwa kwa timu zote mbili, zikiwa na malengo tofauti kwenye msimamo wa ligi.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 46, huku Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya 15 kwa pointi 14. Wekundu wa Msimbazi wanahitaji ushindi ili kuendelea kuweka presha kwenye mbio za ubingwa, wakati Prisons ikitafuta matokeo ya kuipa nafuu katika mapambano ya kutoka mkiani.
Simba imetangaza kikosi chake cha kuanza, Kassali akipewa jukumu la kulinda lango, huku Duchu, Mligo, Vedastus na Toure wakianza katika safu ya ulinzi. Eneo la kati litakuwa na Kagoma, Gueye, Kante na Mwalimu, wakati nahodha Chama na Morice wakitarajiwa kuongoza mashambulizi.
Kwenye benchi, Simba imewataja Abel, Chasambi, Kibabage, Semfuko, Dira, Ned, Baraka, Inno, Mpanzu na Bashir.
Simba inaingia kwenye mchezo huu ikitoka kushinda bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania. Hata hivyo, timu hiyo imelazimika kuhamia KMC Complex baada ya awali kutumia Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
Kwa upande wa Tanzania Prisons, mchezo huu unakuja katika kipindi kigumu. Timu hiyo imepoteza mechi nne kati ya tano za mwisho dhidi ya Mbeya City, TRA United, Yanga na Singida Black Stars, huku ikitoka sare moja dhidi ya KMC. Ushindi wake wa mwisho ulikuwa Februari 14, 2026, ilipoifunga Namungo mabao 3-2 nyumbani.
Fuatilia Matokeo ya Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026 Live
| Simba Sc | VS | Tanzania Prisons |
Muktadha wa Mchezo
Historia ya kukutana kwa Simba na Tanzania Prisons inaonyesha Simba imekuwa na rekodi bora zaidi. Timu hizo zimekutana mara 19 kwenye ligi, Simba ikishinda mechi 12, Tanzania Prisons ikishinda nne, huku mechi tatu zikimalizika kwa sare.
Simba pia imekuwa na mwendo mzuri katika mechi tano za mwisho, ikishinda dhidi ya JKT Tanzania, Namungo na Fountain Gate, pamoja na sare dhidi ya Yanga na TRA United. Matokeo hayo yanaifanya iingie uwanjani ikiwa na morali ya kuendelea kusaka pointi muhimu.
Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema hawauchukulii mchezo huo kirahisi licha ya Tanzania Prisons kuwa katika nafasi ya chini kwenye msimamo.
“Siku zote hakuna mechi rahisi kati yetu Simba na Prisons, mechi hii itakuwa ngumu, tumejipanga kukabiliana na ugumu huo, tumejiandaa vizuri kutafuta ushindi ili kuendelea kuutafuta ubingwa msimu huu,” alisema Matola.
Simba itawakosa wachezaji wawili katika mchezo huu. Nahodha Shomari Kapombe ni majeruhi, huku winga Anicet Oura, licha ya kurejea mazoezini, akitajwa kutokuwa na uwezekano mkubwa wa kucheza leo.
Presha kwa Tanzania Prisons
Kwa Tanzania Prisons, mchezo huu unabeba maana kubwa kutokana na nafasi yake kwenye msimamo. Hata kama itashinda, bado itaendelea kubaki nafasi ya 15 kutokana na tofauti ya pointi dhidi ya Mbeya City, iliyo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 21.
Kocha wa Prisons, Shadrack Nsajigwa, amekiri timu yake haipo katika nafasi nzuri, lakini amesisitiza kuwa bado wanaendelea kupambana kutafuta matokeo.
“Nikweli hatupo kwenye nafasi nzuri lakini hatuna nafasi ya kukata tamaa, lolote linaweza kutokea, haitakuwa mechi rahisi kwetu dhidi ya Simba lakini tumejiandaa kukabiliana nao, tunataka kutafuta pointi yoyote kesho (leo),” alisema Nsajigwa.
Mchezo wa leo unaiweka Simba katika mtihani wa kuendeleza kasi yake kwenye mbio za ubingwa, huku Tanzania Prisons ikihitaji kupambana kwa nguvu kupata pointi katika kipindi kigumu. Matokeo ya Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026 yatasubiriwa kwa karibu kutokana na umuhimu wa mchezo huu kwa pande zote mbili.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026
- Kikosi cha Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026
- Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026 Saa Ngapi?
- Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/05/2026
- Yanga Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mrithi wa Pedro
- Mambo 6 Yaliyosababisha Pedro Kufungashiwa Vilago Yanga
- Harry Kane Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Ligi ya Mabingwa Ulaya
- Rasmi: Simba SC Yahamishia Michezo ya Nyumbani Uwanja wa KMC






Leave a Reply