Mabao ya Allan Okello na Maxi Nzengeli Yaipa Yanga Ushindi Dhidi ya Coastal Union

Mabao ya Allan Okello na Maxi Nzengeli Yaipa Yanga Ushindi Dhidi ya Coastal

Yanga imeendeleza kasi yake katika Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, kwenye mchezo uliopigwa Jumamosi ya tareh 09 mei  2026 katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Mabao mawili ya kiungo Allan Okello dakika ya 18 na 63, pamoja na bao la Maxi Nzengeli dakika ya 75, yalitosha kuipa Yanga pointi tatu muhimu na kuifanya kufikisha jumla ya pointi 54 baada ya kucheza mechi 22 za ligi msimu huu.

Star Boy Okello aliifungia Yanga bao la kwanza baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mwana wa Mfalme Prince Dube, na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili, Pacome Zouzoua alimkuta Okello kwa pasi akiwa nje kidogo ya boksi, kabla ya kiungo huyo kuachia shuti lililomshinda kipa wa Coastal Union, Chuma Ramadhan, na kujaa wavuni.

Baadaye Okello aliendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye mchezo huo baada ya kumpa pasi Maxi Nzengeli, ambaye alifunga bao la tatu na kuhitimisha ushindi wa Yanga.

Ushindi huo umemfanya Okello kufikisha mabao matano na asisti saba msimu huu, huku Yanga ikiendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Mabao ya Allan Okello na Maxi Nzengeli Yaipa Yanga Ushindi Dhidi ya Coastal

Mchango wa Okello na Maxi Katika Ushindi wa Yanga

Okello alikuwa mhusika mkuu katika ushindi huo baada ya kufunga mabao mawili na kutoa pasi ya mwisho kwenye bao la Maxi. Bao lake la kwanza lilitokana na pasi ya Prince Dube, wakati la pili lilitokana na pasi ya Pacome Zouzoua.

Maxi naye alikamilisha kazi ya Yanga dakika ya 75 baada ya kutumia pasi ya Okello, na kuifanya timu hiyo kumaliza mchezo ikiwa na ushindi wa mabao 3-0.

Matokeo hayo pia ni ushindi wa kwanza kwa Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin ‘Master Lecturer’, tangu alipoteuliwa kuiongoza timu hiyo Mei 6, 2026, akichukua nafasi ya Pedro Goncalves.

Yanga Yaendelea Kujigonglea Misumari Kileleni, Coastal Union Yapoteza Tena

Yanga imefikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 22 za Ligi Kuu Bara. Kabla ya kuondoka kwa Pedro, timu hiyo ilikuwa imecheza mechi 21, ikishinda 15 na kutoka sare sita, ikiwa na mabao 47 ya kufunga na kuruhusu matano.

Pedro aliondoka baada ya kukaa ndani ya kikosi hicho kwa siku 193 tangu alipotambulishwa rasmi Oktoba 25, 2025. Katika mechi 19 za Ligi Kuu Bara alizoiongoza Yanga, alishinda 14 na kutoka sare tano, huku timu ikifunga mabao 44 na kuruhusu matano.

Kwa upande wa Coastal Union, kipigo hicho ni cha pili mfululizo baada ya kupoteza mabao 3-2 dhidi ya Fountain Gate Mei 5, 2026. Pia ni kichapo cha pili kwa kocha Fikiri Elias tangu alipoteuliwa Aprili 10, 2026.

Fikiri alianza kwa ushindi katika mechi zake mbili za kwanza dhidi ya Dodoma Jiji na Singida Black Stars, kabla ya kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Fountain Gate na Yanga.

Coastal Union sasa imecheza mechi 22, ikishinda tano, kutoka sare saba na kupoteza 10. Timu hiyo ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 22.

Yanga pia ilijizolea pointi zote tatu katika mchezo wao wa raundi kwanza dhidi ya Coastal Union uliopigwa Desemba 7, 2025, kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Katika mchezo huo, Prince Dube aliifungia Yanga bao pekee dakika ya 88.

Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union umeipa Yanga mwendelezo mzuri chini ya Moallin, huku Allan Okello akiendelea kuwa mmoja wa wachezaji waliochangia moja kwa moja matokeo ya timu hiyo kwa mabao na pasi za mwisho.

Soma Pia:

  1. Matokeo ya Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026
  2. Kikosi cha Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026
  3. Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026 Saa Ngapi?
  4. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/05/2026
  5. Yanga Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mrithi wa Pedro
  6. Mambo 6 Yaliyosababisha Pedro Kufungashiwa Vilago Yanga
  7. Harry Kane Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Ligi ya Mabingwa Ulaya
  8. Rasmi: Simba SC Yahamishia Michezo ya Nyumbani Uwanja wa KMC
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo