Matokeo ya Yanga vs FC Augsburg Leo 20 Julai 2024: Mpumalanga Cup | Matokeo ya Yanga Dhidi ya Augsburg Leo
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara mara tatu mfululizo klabu ya Yanga leo itakutana na mabingwa wa soka kutoka Ujerumani, FC Augsburg, katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kirafiki ya Mpumalanga Premier’s International Cup. Mechi hii itafanyika katika uwanja wa Mbombela, uwanja uliowahi kutumika kwenye Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2010.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wanasubiri kwa hamu matokeo ya mchezo huu. Yanga, wakiwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kombe la shirikisho (CRDB Bank federation cup), wataonyesha uwezo wao dhidi ya timu kubwa kutoka Bundesliga ya Ujerumani. FC Augsburg nao watajaribu kuonyesha ubabe wao kutoka Ulaya.
Katika mechi hii, Yanga itawatambulisha wachezaji wao wapya, akiwemo nyota wa zamani wa Simba SC Clatous Chama, aliyejiunga na timu ya Wananchi Jangwani kwa mkataba wa miaka miwili. Pia kutakuwa na Prince Dube na Jean Baleke ambao watakuwa wakicheza mechi yao ya kwanza wakiwa na jezi ya Yanga. Mashabiki wamekuwa na hamu kubwa ya kuona jinsi nyota hawa wapya watakavyocheza pamoja na wachezaji mahiri kama Stephane Aziz Ki, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua na wengineo.
Matokeo ya Yanga vs FC Augsburg Leo 20 Julai 2024
FC Augsburg | 2-1 | Yanga Sc |
- Daki: 13 Matokeo ni 0-0
- Daki: 18 Matokeo ni 0-0
- Daki: 31 Matokeo ni 0-0
- Daki: 36 Matokeo ni 1-0
- Daki: 45 Matokeo ni 1-0, Kipindi cha Kwanza Kimemalizika
- Daki: 46 Matokeo 1-0
- Daki: 52 Matokeo 1-0
- Daki: 65 Matokeo 1-0
- Daki: 80 Matokeo 2-0
- Daki: 90 Matokeo 2-1 (Goal By Baleke)
- Mpira Umemalizika; 2-1
Taarifa Kuhusu Mechi ya Yanga Dhidi ya FC Augsburg
🏆 #MpumalangaCup🇿🇦
⚽️ FC Augsburg🇩🇪🆚Young Africans SC🇹🇿
📆 20.07.2024
🏟 Mbombela Stadium
🕖 15H00🇿🇦 16H00🇹🇿
Vikosi Mechi ya Matokeo ya Yanga vs FC Augsburg Leo 20 Julai 2024
Kikosi cha Yanga
- Kikosi cha Kinachoanza: 39 Diarra, 21 Yao, 30 Kibabage, 5 D. Job, 4 Bacca, 18 Sureboy, 7 Maxi, 27 Mudathir, 24 Clement, 17 Chama & 10 Aziz Ki
- Wachezaji wa Ziada: Khomeny, Mwamnyeto, Aziz A., Boka, Mkude, Duke, Shekhan, Dube & Baleke
Kikosi cha FC Augsburg
- Kikosi Kinachoanza: 25 Klein, 3 Pedersen, 6 Gouweleeuw, 8 Rexhbecaj, 15 Mounié, 18 Breithaupt, 24 Jensen, 27 Engels, 29 Essende, 31 Schlotterbeck & 44 Koudossou
- Wachezaji wa Ziada (Subs): 33 Jäger, 5 Pfeiffer, 7 Kabadayi, 10 Maier, 11 Mbuku, 14 Okugawa, 21 Tietz, 23 Bauer, 30 Dorsch, 36 Kömür, 37 Petkov, 40 Banks & 48 Cardona
Baada ya burudani ya soka la vilabu kutoweka kwa wiki kadhaa, Hatimaye mashabiki wa Yanga sasa watapata nafasi ya kuishuhudia klabu yao pidwa ikikipiga na wababe kutoka Ujerumani katika Uwanja wa Mbombela ambapo historia itaandikwa, kwani huu utakuwa mchezo wa kwanza wa FC Augsburg wa kufanya maandalizi ya msimu mpya nje ya bara la Ulaya.
Wajerumani hawa watakuwa nchini Afrika Kusini kuanzia tarehe 18 hadi 28 Julai, wakitumia fursa hii kujiandaa kwa msimu mpya wa Bundesliga. Mechi hii pia itakuwa maalum kwa Stephane Aziz Ki, kiungo mshambuliaji wa Yanga.
Aziz Ki anakumbukwa kwa tukio la bao lake la utata dhidi ya Mamelodi Sundowns kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita. Huu utakuwa mchezo wake wa kwanza kurudi Afrika Kusini tangu tukio hilo.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply