Kikosi cha Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025 | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya Stellenbosch Kombe la Shirikisho
Kikosi cha wekundu wa Msimbazi, Simba, kinatarajiwa kushuka dimbani leo, Jumapili, Aprili 20, 2025, visiwani Zanzibar kwa ajili ya kukipiga na timu ya Stellenbosch ya Afrika Kusini katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mechi hii itachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, baada ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungiwa kwa ukarabati. Mchezo huu utakuwa na mvuto mkubwa huku mashabiki wakitarajia kuona timu zao zikionyesha umahiri wa kisoka katika uwanja wa New Amaan.
Mchezo huu wa nusu fainali unakuja na motisha ya kipekee kwa wachezaji wa kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba kutoka kwa mfadhili wa zamani, Azim Dewji, ambaye ameahidi kuongeza dau la fedha kwa kila bao na asisti.
Katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Masry, Azim alitoa ahadi ya Sh2.5 milioni kwa kila bao na asisti, lakini kwa mechi hii ya nusu fainali, kiwango hicho kimeongezeka mara mbili. Wachezaji sasa watajivunia Sh6 milioni kwa kila asisti na Sh12 milioni kwa kila bao, huku mgawanyo wa fedha ukifanyika kwa usawa, ambapo mfungaji atapata Sh6 milioni na mchezaji atakayetoa pasi atapata kiasi hicho hicho.
Azim alieleza kuwa ahadi hii inalenga kuongeza msukumo kwa wachezaji na kuhakikisha kuwa timu inapata matokeo bora.
“Wachezaji walifurahia kile kilichofanyika katika mchezo uliopita na wanataka kufunga mabao mengi zaidi ili kufanya mchezo wa marudiano uwe rahisi kwetu,” alisema Azim. Ahadi hii ya fedha inatolewa kwa lengo la kuhamasisha wachezaji kutoa mchango wao wa juu na kutengeneza ushindi mkubwa dhidi ya Stellenbosch.
Kikosi cha Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025
Kikosi rasmi cha Simba kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 09:00 jioni. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Faldu Davis atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo Stellenbosch itakua na jukumu la kuonesha ubabe wake ugenini, huku Simba ikipambana kuendeleza rekodi yake nzuri inapokua uwanja wa nyumbani.
Simba inahitaji msaada wa mashabiki wao ili kuhakikisha wanapata matokeo bora leo. Azim Dewji pia amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanja wa New Amaan, Zanzibar, na kuonyesha upendo na hamasa kwa wachezaji wao. “Tunataka kuwaona mashabiki wakiwa wameshika usukani wa kuhamasisha vijana wetu ili wafanye vizuri uwanjani. Huu ni wakati wa kushirikiana na timu yetu ili kufikia malengo yetu,” alisema.
Kocha wa Simba, Fadlu Davids, amekuwa akifanya kazi nzuri na timu yake huku akiongoza kikosi hicho kwa mafanikio makubwa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Azim Dewji pia alitumia fursa hii kutaja juhudi za benchi la ufundi na uongozi wa klabu, akisema, “Nina imani na timu kuanzia benchi la ufundi linalofanya kazi nzuri chini ya Fadlu Davids. Simba inashinda kwa ubora uwanjani na inasonga mbele.”
Mechi ya Marudiano na Maendeleo ya Simba
Mchezo wa leo ni muhimu kwa Simba, kwani ushindi utawapa nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mshindi wa jumla atakuwa na nafasi ya kwenda ugenini kwa mchezo wa marudiano, na Simba inahitaji kupata matokeo mazuri ili kucheza kwa urahisi kwenye mchezo huo wa marudiano. Mashabiki na wachezaji wanatarajiwa kujitolea kwa hali ya juu ili kufikisha timu kwenye fainali, na kwa sasa kila kitu kinategemea matokeo ya mechi hii ya nusu fainali.
Simba inajiandaa kwa kivumbi hiki cha kihistoria, na mashabiki wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kutoa sapoti kwa timu yao. Hii ni fursa ya kipekee kwa timu ya Simba kutimiza ndoto yao ya kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, na wachezaji wanahamasishwa na dau kubwa linalotolewa na Azim Dewji.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025 Saa Ngapi?
- Dickson Ambundo Ajiondoa Fountain Gate Akidai Kutolipwa Zaidi ya Shilingi Milioni 50
- Viingilio Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
- Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
- Kikosi cha Stellenbosch Chawasili Zanzibar kwa Ajili ya Simba
- Ratiba ya Mechi za Leo 19/04/2025 Ligi Kuu NBC
- Msigwa Afunguka Kuhusu Ukarabati wa Uwanja wa Mkapa
Leave a Reply