Aliekua Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya

Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya

Aliekua Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya

Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili tangu alipoachana na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, kocha raia wa Argentina, Miguel Gamondi, sasa ametua rasmi nchini Libya kujiunga na klabu ya Al Nasr. Hatua hii inamfanya kurejea rasmi kwenye benchi la ufundi, akilenga kusaidia timu hiyo kufanikisha malengo yake katika mashindano ya ndani na nje ya nchi hiyo.

Aliekua Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya

Mkataba Mpya wa Gamondi na Al Nasr

Taarifa kutoka Libya zinaeleza kuwa Gamondi amesaini mkataba wa miezi sita na Al Nasr hadi mwishoni mwa msimu huu. Aidha, mkataba huo unajumuisha kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi endapo atafanikisha malengo ya klabu hiyo kwenye michuano inayowakabili. Ujio wake unaleta matumaini makubwa kwa Al Nasr, timu inayojitahidi kujiimarisha katika ligi ya Libya na mashindano ya kimataifa.

Historia ya Gamondi na Yanga SC

Gamondi alijiunga na Yanga SC mnamo Juni 24, 2023, akichukua nafasi ya Mtunisia Nasreddine Nabi. Akiwa na klabu hiyo ya Jangwani, aliweza kuiongoza katika jumla ya michezo 40 ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya msimu wa 2023-2024 na 2024-2025. Katika kipindi hicho, Gamondi alishinda michezo 34, kutoka sare mara mbili na kupoteza minne pekee. Pia, alifanikiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga kufunga jumla ya mabao 85 huku timu yake ikiruhusu mabao 18 pekee.

Mafanikio Yake Akiwa na Kikosi Cha Yanga

Kocha huyo alichangia mafanikio makubwa kwa Yanga SC, akiwasaidia kushinda mataji matatu muhimu, ikiwemo:

  • Taji la Ligi Kuu Tanzania Bara 2023-2024, ambalo liliifanya Yanga kufikisha jumla ya mataji 30 tangu mwaka 1965.
  • Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) 2024
  • Ngao ya Jamii 2024

Aidha, Gamondi aliifikisha Yanga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1998, ikiwa ni mafanikio makubwa kwa klabu hiyo kwenye michuano hiyo ya kimataifa.

Sababu za Kuachana na Yanga

Licha ya mafanikio hayo, Gamondi aliachana na Yanga mnamo Novemba 15, 2024, baada ya msururu wa matokeo yasiyoridhisha katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Timu hiyo ilipoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Azam FC kwa 1-0 mnamo Novemba 2, kisha kupoteza 3-1 dhidi ya Tabora United mnamo Novemba 7. Katika kipindi hicho, Yanga ilikuwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 24. Hatua hiyo ilipelekea klabu kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi, na nafasi yake kuchukuliwa na kocha Mjerumani, Saed Ramovic.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kagera Sugar Yatamba Kuondoa Unyonge KMC Complex Dhidi ya Yanga
  2. Morocco Aweka Mikakati ya Ushindi dhidi ya Vigogo Ndani ya Kundi C AFCON 2025
  3. Simba SC Yajiandaa Vikali Kuisambaratisha Tabora United
  4. Makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2025
  5. Tanzania Yapangwa Kundi C AFCON 2025
  6. Kundi la Taifa Stars AFCON 2025
  7. Timu zilizofuzu 32 bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
  8. Kundi la Stars AFCON 2025 Kufahamika Leo
  9. Ramovic Aelezea Sababu za Ikanga Kukosa Mchezo wa Kombe la Shirikisho
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo