Matokeo ya Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025

Simba SC vs CS Constantine Leo 19 01 2025

Matokeo ya Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025 | Matokeo ya Mechi ya Simba Leo Dhidi ya CS Constantine

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup), Simba SC, leo wanatarajia kushuka dimbani kuivaa CS Constantine ya Algeria katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mchezo huo ni wa kuamua nani ataongoza Kundi A, huku Simba wakiwa na dhamira ya kulipa kisasi kwa wapinzani wao baada ya kufungwa 2-1 katika mchezo wa awali uliochezwa Algeria.

Mchezo huu utaanza kutimua vumbi leo, 19 Januari 2025, majira ya saa 10:00 jioni. Ingawa utachezwa bila mashabiki, nyota wa Simba SC wameonyesha kujiamini kwa kutangaza wazi kuwa wanataka ushindi wa nyumbani ili kumaliza hatua ya makundi wakiwa vinara. Kwa sasa, Simba wanashika nafasi ya pili katika Kundi A wakiwa na alama 10, wakifuatiwa na CS Constantine wenye alama 12. Ushindi kwa Simba leo utawafanya wafikishe alama 13 na kuongoza kundi hilo.

Kocha wa Simba, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa wataingia uwanjani kucheza mpira wao wa kawaida bila presha, huku akilenga ushindi ili kuepuka kukutana na timu ngumu kama Zamalek au Al Masry katika hatua inayofuata. “Ni muhimu kumaliza vinara wa kundi ili kujiweka katika nafasi nzuri kwa hatua zijazo. Tunaamini uwezo wetu na tupo tayari kwa changamoto yoyote,” alisema Davids.

Matokeo ya Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025

Matokeo ya Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025

Simba Sc VS CS Constantine

Mbinu na Maandalizi

Kwa upande wa wachezaji, nahodha Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na mlinzi Jean Charles Ahoua wamesema kuwa wamejiandaa vya kutosha kuwakabili wapinzani wao. Wachezaji hao wameweka wazi kuwa dhamira yao ni kulipiza kisasi cha kipigo cha 2-1 walichopokea walipokutana na CS Constantine ugenini.

Katika mchezo huo wa awali, Simba walitangulia kufunga bao kupitia Mohammed Hussein, lakini makosa ya dakika tano katika kipindi cha pili yaliwapa CS Constantine ushindi. Katika mchezo wa leo, Simba wanapanga kutumia kikamilifu faida ya kucheza nyumbani kwa kushambulia zaidi na kuhakikisha wanadhibiti mchezo.

Rekodi na Taarifa za Kundi

Ikumbukwe kuwa, hii ni mara ya pili tu kwa Simba kufikia hatua ya kumaliza makundi wakiwa vinara. Mara ya kwanza ilikuwa msimu wa 2020/2021 walipoongoza Kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa alama 13. Ushindi wa leo pia utaiweka Simba katika rekodi ya kuwa na asilimia 100 ya ushindi katika mechi za nyumbani za kimataifa msimu huu.

Kwa upande wa rekodi za wapinzani, CS Constantine wameonyesha umahiri mkubwa ugenini kwa kucheza kwa mbinu ya kuvizia. Hii inamaanisha Simba inapaswa kuwa makini na kushambulia kwa tahadhari ili kuepuka mashambulizi ya kushtukiza.

Mwamuzi wa Mchezo

Mchezo wa leo utachezeshwa na mwamuzi Celso Armindo Alvacao kutoka Msumbiji, anayejulikana kwa kutoa kadi nyingi. Katika rekodi zake za mechi 21 za kimataifa, ametangaza jumla ya kadi 83, huku timu za nyumbani mara nyingi zikiwa na bahati ya kushinda. Hii inaweza kuwa ishara nzuri kwa Simba ikiwa watadhibiti mchezo bila kufanya makosa.

Mapendekezo ya Mhariri;

  1. Kikosi cha Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025
  2. Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024 Saa Ngapi?
  3. Matokeo ya Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024
  4. Kocha MC Alger Atamba Kupata Pointi 3 Dhidi ya Yanga Licha ya Joto Kali
  5. Ligi Kuu Bara Kurejea Februari kwa Moto! Simba na Yanga Kuanza na Viporo
  6. Mtibwa Sugar Kuwakaribisha Azam FC Manungu kwa Mechi ya Kirafiki
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo