Matokeo ya Kidato Cha Pili 2024 | Matokeo ya Form Two 2024
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha Pili kwa mitihani iliyofanyika mwezi Oktoba/Novemba 2024. Takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 680,574 kati ya 796,825 waliopimwa, ambao ni sawa na asilimia 85.41%, wamefaulu na kuendelea na Kidato cha Tatu baada ya kufikia madaraja I, II, III, na IV. Matokeo haya yametangazwa leo, Januari 4, 2025, jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed.
Kwa mujibu wa Dkt. Mohamed, mwaka 2023 jumla ya wanafunzi 592,741 walifaulu, ikiwa ni asilimia 85.31%. Hii inaonyesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 0.10%. Kati ya wanafunzi 680,574 waliofaulu mwaka 2024, wasichana ni 367,457 sawa na asilimia 83.99%, huku wavulana wakiwa 313,117 sawa na asilimia 87.13%. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa wavulana wameendelea kuongoza kwa ufaulu bora ikilinganishwa na wasichana.
Wanafunzi wa Kujitegemea Waweka Historia
Kwa mara ya kwanza, wanafunzi wa kujitegemea walishiriki katika upimaji wa kitaifa wa Kidato cha Pili. Kati ya hao, wanafunzi 4,205 sawa na asilimia 55.94%, wamefaulu na sasa wanastahili kufanya mtihani wa Kidato cha Nne. Hii ni hatua muhimu inayodhihirisha juhudi za NECTA katika kuwajumuisha wadau mbalimbali wa elimu nchini.
Changamoto za Udanganyifu na Hatua Zilizochukuliwa
NECTA pia imechukua hatua za kisheria dhidi ya udanganyifu uliojitokeza wakati wa mitihani. Matokeo ya wanafunzi 41 wa Kidato cha Pili na 100 wa Darasa la Nne yamefutwa kutokana na udanganyifu, huku wengine watano wakifutiwa matokeo kwa kuandika lugha isiyofaa kwenye skripti zao za mtihani. Hatua hizi zimechukuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5(2)(j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani, Sura ya 107, kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2)(b) cha Kanuni za Mitihani za mwaka 2016.
Umuhimu wa Mtihani wa Kidato cha Pili (FTNA)
Mtihani wa Kidato cha Pili, unaojulikana kama Form Two National Assessment (FTNA), ni mojawapo ya mitihani muhimu inayosimamiwa na NECTA. Mtihani huu hufanyika kila mwaka kwa wanafunzi wa shule za sekondari kote Tanzania.
Lengo kuu ni kupima uelewa wa wanafunzi baada ya miaka miwili ya masomo na kutoa mrejesho kwa walimu, wanafunzi, na wadau wa elimu kuhusu maeneo ya kuboresha mbinu za kufundisha na kujifunza.
Mtihani wa FTNA unahusisha masomo mbalimbali, yakiwemo:
- Kiswahili
- Hisabati
- Kiingereza
- Biolojia
- Fizikia
- Kemia
- Jiografia
- Historia
- Elimu ya Dini (Kiislamu na Kikristo)
- Uraia
- Masomo ya Ufundi na Biashara
- Lugha za Kigeni (Kifaransa, Kichina, n.k.)
Mwongozo wa Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Pili 2024
Wanafunzi na wadau wa elimu wanaweza kupata matokeo haya kupitia tovuti rasmi ya NECTA kwa hatua zifuatazo:
- Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA
Fungua kivinjari cha intaneti na tembelea anwani ya www.necta.go.tz. Hakikisha una mtandao imara. - Chagua Sehemu ya “Results”
Bofya kitufe cha “Results” kwenye menyu kuu ili kufikia orodha ya mitihani yote inayosimamiwa na NECTA. - Chagua “FTNA” (Form Two National Assessment)
Tafuta na bofya FTNA ili kufungua ukurasa wa matokeo ya Kidato cha Pili. - Chagua Mwaka wa Mtihani
Baada ya kufungua FTNA, chagua mwaka wa mtihani, yaani 2024. - Tafuta Jina la Shule
Tafuta jina la shule yako ili kuonyesha matokeo ya wanafunzi wote wa shule husika. - Tafuta Jina la Mwanafunzi au Namba ya Mtihani
Tumia kipengele cha utafutaji kutafuta jina la mwanafunzi au namba ya mtihani. Matokeo yataonyesha jina la mwanafunzi, alama za kila somo, jumla ya alama, na daraja la ufaulu (Division).
Kwa habari zaidi, tembelea tovuti ya NECTA au wasiliana na shule husika kwa maelezo ya kina.
Pia Unaweza kuangalia matokeo ya kidato cha pili 2024 moja kwa mija kupitia viungo vilivyopo hapa chini
ARUSHA | MOROGORO |
DAR ES SALAAM | MTWARA |
DODOMA | MWANZA |
GEITA | NJOMBE |
IRINGA | PWANI |
KAGERA | RUKWA |
KATAVI | RUVUMA |
KIGOMA | SHINYANGA |
KILIMANJARO | SIMIYU |
LINDI | SINGIDA |
MANYARA | SONGWE |
MARA | TABORA |
MBEYA | TANGA |
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply