Msuva Asubiri Mkataba Mpya Mnono Al-Talaba SC
Duru za usajili zimejaa minong’ono kuhusu mshambuliaji mwenye ubora wa hali ya juu wa Tanzania, Simon Msuva, ambaye kwa sasa anasubiri ofa ya mkataba mpya wa miaka miwili na klabu yake ya Al-Talaba SC ya Iraq. Hii ni baada ya mkataba wake wa sasa kukalibia kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, mabosi wa Al-Talaba SC wameonyesha nia thabiti ya kumshawishi Msuva kuendelea kuwatumikia, wakizingatia mchango wake mkubwa tangu alipojiunga nao. Licha ya mafanikio aliyoyapata akiwa na Al-Talaba, uvumi umeanza kuenea kuwa klabu nyingine kadhaa za Ligi Kuu ya Iraq zimeanza kuonyesha nia ya kumshawishi kujiunga nao.
Sababu ya Al-Talaba Kutaka Kumweka Msuva
Tangu alipojiunga na Al-Talaba SC, Simon Msuva amekuwa mhimili muhimu wa timu hiyo. Mpaka sasa, amefunga mabao mawili na kutoa asisti moja kwenye michezo ya Ligi Kuu ya Iraq, kiwango kilichowavutia viongozi wa klabu hiyo na mashabiki pia. Kasi yake, nidhamu, na maarifa ya kiufundi vimemfanya kuwa mchezaji wa kutegemewa sana katika kikosi cha Al-Talaba SC.
Pamoja na hayo, mafanikio yake haya yameanza kuvutia macho ya klabu nyingine. Moja ya klabu zinazotajwa kuwa na nia ya kumsajili ni Naft Al-Basra SC, ambayo tayari imeweka wazi mpango wa kuboresha kikosi chao katika dirisha dogo la usajili.
Kauli ya Simon Msuva Kuhusu Mkataba Mpya
Licha ya taarifa nyingi kuibuka kuhusu mkataba wake mpya, Simon Msuva amesisitiza kuwa bado hajapokea ofa rasmi kutoka kwa Al-Talaba SC. Hata hivyo, ameonyesha kufurahia jinsi kazi yake inavyothaminiwa, akisema:
“Sijapata taarifa rasmi kuhusu hilo, lakini ni jambo zuri kuona watu wanaanza kuthamini kile ninachofanya. Hii inanipa motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi.”
Kauli hii inaonyesha kuwa Msuva amejiweka tayari kwa changamoto mpya, huku akithamini nafasi aliyonayo ndani ya Al-Talaba SC.
Mafanikio ya Msuva Nje ya Klabu: Mbali na mafanikio yake ndani ya Al-Talaba SC, Simon Msuva amekuwa lulu kwa taifa lake pia. Hivi karibuni, alisaidia Taifa Stars kufuzu kwa mara ya nne katika fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON). Hili limezidi kuimarisha jina lake si tu nchini Tanzania, bali pia kwenye anga za kimataifa.
Kwa sasa, hali ya mshambuliaji huyo iko mikononi mwa Al-Talaba SC. Mashabiki wa klabu hiyo wana matarajio makubwa kuona Msuva akisaini mkataba mpya, kwani mchango wake umetengeneza pengo kubwa ambalo si rahisi kuziba. Hata hivyo, klabu nyingine zikiwemo Naft Al-Basra SC zinaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya nyota huyo.
Ikiwa Al-Talaba itashindwa kumshawishi kusaini mkataba mpya, kuna uwezekano mkubwa wa kuona Msuva akihamia klabu nyingine yenye mipango thabiti ya kumtumia kikamilifu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kocha Kagera amsifu Charles Boniface Mkwasa: ‘Kocha bora nchini’
- Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
- Matokeo ya Simba vs FC Bravos do Maquis leo 27/11/2024
- Yanga Yaanza Makundi Klabu Bingwa Kwa Kichapo Cha Aibu Nyumbani
- Kikosi cha Simba vs FC Bravos do Maquis leo 27/11/2024
- Mechi ya Simba vs FC Bravos do Maquis leo 27/11/2024 Saa Ngapi?
- Singida Black Stars Yawatumbua Makocha Aussems na Kitambi!
- Ratiba ya yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025
- Ratiba ya Makundi Klabu Bingwa CAF 2024/2025
Leave a Reply