Yanga Yatangaza Kumsajili Duke Abuya

Yanga Yatangaza Kumsajili Duke Abuya

Yanga Yatangaza Kumsajili Duke Abuya: Klabu ya Yanga imezidi kuimarisha kikosi chake kwa kutambulisha kiungo wa boli Duke Abuya kuelekea msimu wa 2024/2025. Hii ni hatua muhimu kwa klabu ambayo imekuwa ikijiandaa kwa muda mrefu kuhakikisha inakuwa na kikosi imara kinachoweza kushindana katika michuano yote, ndani na nje ya nchi. Hatua hii ya kumsajili Abuya inakuja baada ya uvumi uliodumu kwa wiki kadhaa kuhusu uhamisho wake.

Yanga Yatangaza Kumsajili Duke Abuya

Yanga Yatangaza Kumsajili Duke Abuya

Duke Abuya, ambaye ametambulishwa rasmi na timu ya wananchi akitokea Sigida Black Stars (Ihefu SC), ni mchezaji mwenye uwezo wa kipekee wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani. Anajulikana kwa uwezo wake wa kucheza kama kiungo mkabaji, kiungo mshambuliaji, na hata winga wa kulia. Uwezo wake wa kucheza katika nafasi hizi tofauti unampa kocha wa Yanga Miguel Ángel Gamondi chaguo zaidi katika kupanga kikosi, hasa wakati wa mechi muhimu.

Abuya anakua mchezaji wa sita kuongezwa katika kikosi cha Yanga kuelekea msimu wa 2024/2025. Wachezaji wengine ambao wameshatambulishwa na klabu ni pamoja na Clatous Chama, Prince Dube, Boka Chadrak, Khomeini Abubakar na Aziz Andabwile

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Azam Yatuma Ofa Kwa Simba Kumsajili Kipa Aishi Manula
  2. Stephane Aziz Ki Asaini Mkataba Mpya na Yanga SC
  3. Mshahara Wa Stephane Aziz Ki Yanga 2024/2025
  4. CV ya Valentin Nouma: Sifa Zote za Beki Mpya Simba 2024/2025
  5. Cv ya Karaboue Chamou Beki Mpya Wa Simba 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo