Yanga Yapata Mserereko CAF: Mechi Zote za Klabu Bingwa Kupigwa Dar es Salaam
Katika habari zitakazowafurahisha mashabiki wa soka nchini Tanzania, klabu ya Yanga SC imepata mserereko mkubwa katika kampeni yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Klabu ya Vital’O ya Burundi, wapinzani wa Yanga katika hatua ya awali, imehamishia mechi yao ya nyumbani kuchezwa nchini Tanzania. Hii ina maana kwamba Yanga watacheza mechi zote mbili za hatua ya awali ndani ya ardhi ya nyumbani.
Yanga itaanza kampeni yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’O FC ya Burundi katika hatua ya awali. Awali, mechi ya mkondo wa kwanza ilipangwa kuchezwa ugenini, lakini kutokana na hali ya uwanja, mechi zote mbili sasa zitachezwa ndani ya ardhi ya Tanzania.
Mkondo wa kwanza wa mchezo unatarajiwa kupigwa kati ya Agosti 16 na 18 kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Mkondo wa pili utapigwa kati ya Agosti 23 na 25 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Hii inamaanisha kuwa Yanga itacheza mechi zake zote za hatua ya awali nyumbani, jambo ambalo ni faida kubwa kwao.
Ratiba ya Mechi
- Mkondo wa Kwanza: Agosti 16-18, Uwanja wa Benjamin Mkapa
- Mkondo wa Pili: Agosti 23-25, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Faida kwa Yanga
Kuwa na mechi zote mbili nyumbani ni faida kubwa kwa Yanga. Hii itawaruhusu kucheza kwa kujiamini zaidi mbele ya mashabiki wao, jambo ambalo linaweza kuongeza ari yao na kuwasaidia kupata matokeo mazuri.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Tuzo ya Mchezaji Bora Ligi Kuu NBC 2023/2024: Hawa Ndio Wagombea
- Hizi apa Tuzo Anazowania Stephane Aziz Ki
- Wanaowania Tuzo za TFF 2023/2024
- Hizi Apa Picha Za Jezi Mpya Ya Simba 2024/2025
- Hii apa Ratiba ya Mechi za Azam Fc Pre season
- Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Tarehe, Matukio na Bei ya Tiketi
- Novatus Miroshi Ajiunga na Goztepe ya Uturuki
Leave a Reply