Yanga vs Tp Mazembe Leo 14/12/2024 Saa Ngapi?

Yanga vs Tp Mazembe Leo Saa Ngapi

Yanga vs Tp Mazembe Leo 14/12/2024 Saa Ngapi?

Klabu ya Yanga imesafiri kwenda Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kwa ajili ya kukabiliana na TP Mazembe katika mchezo muhimu wa mzunguko wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi. Mechi hiyo itachezwa leo, tarehe 14 Desemba 2024, kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Taarifa kamili Kuhusu Meci ya Yanga vs Tp Mazembe

  • 🏆 #CAFCL
  • ⚽️ TP Mazembe🆚Young Africans SC
  • 📆 14.12.2024
  • 🏟 Stade TP Mazembe
  • 🕖 3pm🇨🇩4pm🇹🇿

Yanga vs Tp Mazembe Leo 14/12/2024 Saa Ngapi?

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesisitiza kuwa mafanikio katika mchezo huu yatategemea juhudi kubwa za wachezaji. Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya safari, Kamwe alisema: “Hakuna historia wala vijisababu vitakavyotusaidia. Hapa ni jasho, damu, na machozi kwa dakika zote 90. Ni muda wa kujituma na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.”

Historia ya Mkutano wa Yanga na TP Mazembe

Yanga na TP Mazembe zimekutana mara mbili katika misimu miwili iliyopita kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo Yanga iliibuka mshindi mara zote mbili. Mnamo Februari 19, 2023, Yanga ilishinda 3-1 dhidi ya TP Mazembe katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kabla ya kushinda tena 1-0 kwenye uwanja wa ugenini huko Lubumbashi.

Hata hivyo, mchezo wa leo ni tofauti kabisa, kwani timu zote mbili zipo kwenye hali ngumu katika kundi lao. TP Mazembe ina alama moja tu baada ya sare ya 0-0 dhidi ya MC Alger, huku Yanga ikiwa haina alama baada ya kupoteza michezo miwili ya awali dhidi ya Al Hilal (2-0) na MC Alger (2-0).

Umuhimu wa Ushindi kwa Yanga

Mchezo wa leo una umuhimu mkubwa kwa Yanga, kwani ushindi ndio njia pekee ya kuendelea kuwa kwenye kinyang’anyiro cha kutinga hatua ya robo fainali. Timu inahitaji kuonyesha ubora wa hali ya juu dhidi ya TP Mazembe, ambayo inajulikana kwa uzoefu wake mkubwa katika mashindano ya kimataifa.

Mapendekezo ya Mahariri:

  1. Miguel Cardoso Akabidhiwa Mikoba ya Ukocha Mamelodi
  2. Viingilio Mechi ya Simba VS CS Sfaxien 15/12/2024
  3. Timu Zinazoshiriki Mapinduzi cup 2025
  4. Ndoa Ya Coastal na Ley Matampi Yavunjika Rasmi
  5. Mapinduzi Cup 2025 Kuchezwa na Timu za Taifa Badala ya Vilabu
  6. Kocha Ramovic Aeleza Sababu za Yanga Kushindwa Mbele ya Waarabu
  7. Yanga Karibu Kumsajili Kelvin Nashon kutoka Singida
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo