Yanga VS Simba Leo 08/03/2025 Saa Ngapi?
Hatimaye ile siku ambayo mashabiki wengi wa soka la Tanzania huisubiri kwa shauku kubwa imewadia, ambapo nchi itasimama kushuhudia pambano la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga. Mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa pande zote kwani utachangia kwa kiasi kikubwa kuamua bingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025.
Taarifa Muhimu za Mchezo wa Yanga Sc vs Simba Sc Leo
- Muda wa Mchezo: Saa 1:15 Usiku (19:15)
- Uwanja: Benjamin Mkapa
- Timu Zinazoshiriki: Young Africans SC 🆚 Simba SC
Za Hivi Punde Mechi ya Leo ya Yanga Dhidi ya Simba Yaahirishwa
Huu ni mchezo wa marudiano baada ya Yanga kushinda mechi ya kwanza kwa bao 1-0. Mashabiki wanatarajia upinzani mkali zaidi, huku Simba wakitaka kulipa kisasi na Yanga wakipambana kulinda rekodi yao.
Tathmini ya Timu Kabla ya Mchezo
Young Africans SC (Yanga)
Yanga itaingia dimbani chini ya kocha wao mpya, Miloud Hamdi, ambaye kwa mara ya kwanza ataiongoza timu yake katika mechi hii kubwa ya watani wa jadi. Bahati nzuri kwake, ana kikosi chenye uzoefu wa mechi za presha kama hii.
Nguvu kubwa ya Yanga inatokana na safu yao ya kiungo, ambapo wachezaji wake wana uwezo wa kuzuia na kutengeneza mashambulizi kwa ufanisi mkubwa. Wachezaji muhimu kama Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Stephanie Aziz Ki, Clatous Chama, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, na Duke Abuya wanaweza kuleta matokeo mazuri kwa Yanga endapo wataweza kudhibiti eneo la kati.
Katika safu ya ushambuliaji, Clement Mzize na Prince Dube ndio tegemeo kubwa la Yanga, ambapo wote kwa pamoja wamefunga mabao 20 msimu huu. Kasi yao inawafanya kuwa hatari kwa mabeki wa Simba, hasa katika mashambulizi ya kushtukiza.
Hata hivyo, Yanga wamekuwa wakifanya makosa katika safu ya ulinzi, jambo linaloweza kuwa hatari endapo Simba watatumia nafasi zao vizuri.
Simba SC
Kwa upande wa Simba, kocha Fadlu Davids ataingia dimbani kwa mara ya tatu msimu huu kupambana na Yanga, baada ya kupoteza michezo miwili ya awali kwa matokeo ya 1-0.
Simba wanategemea nguvu ya mabeki wao wa pembeni, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, ambao wamekuwa wakisaidia mashambulizi kwa kasi kubwa. Hata hivyo, kwenye mchezo huu, watakuwa na changamoto kubwa kwani Yanga ina viungo hatari wanaoweza kutumia nafasi yoyote kudhoofisha safu ya ulinzi ya Simba.
Katika safu ya kiungo, wachezaji kama Ellie Mpanzu, Kibu Denis, na Jean Charles Ahoua wanatarajiwa kuwa mhimili wa timu, hasa katika kutengeneza mashambulizi na kupunguza nguvu ya viungo wa Yanga.
Kwa upande wa safu ya ushambuliaji, Leonel Ateba na Steve Mukwala wamefunga mabao 16 kwa pamoja msimu huu, lakini Simba wanamtegemea zaidi Jean Charles Ahoua, ambaye ndiye kinara wa mabao kwa timu hiyo akiwa na mabao 10 na asisti 6.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Tabora United Kuwakabili JKT Tanzania CCM Kirumba Machi 7, 2025
- Bodi ya Ligi TPLB Yatangaza Tarehe Mpya ya Mechi ya Simba na Dodoma
- Timu Zilizofuzu 16 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup 2024/2025
- Mechi za Yanga Zilizobaki Ligi Kuu NBC 2024/2025
- Ratiba ya Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup Leo 03/03/2025
- Ratiba ya Mechi za Simba Machi 2025
- Mbeya City Yaing’oa Azam CRDB Bank Federation Cup kwa Mikwaju ya Penati
- Simba Yaivuruga Rekodi ya Mwambusi Arusha
Leave a Reply