Yanga vs Pamba Jiji Leo 03/10/2024 Saa Ngapi?

Yanga vs Pamba Jiji Leo 03 10 2024 Saa Ngapi

Mechi ya Yanga vs Pamba Jiji Leo 03/10/2024 Saa Ngapi?

Michuano ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 inaendelea leo tarehe 03 Oktoba 2024, kwa mechi kali itakayowakutanisha mabingwa watetezi, Yanga SC, dhidi ya Pamba Jiji FC kwenye dimba la Azam Complex jijini Dar es Salaam. Mchezo huu unatarajiwa kuanza majira ya saa 12:30 jioni (saa 6:30 PM kwa muda wa Afrika Mashariki).

Muhtasari wa Mechi:

  • Timu: Yanga SC 🆚 Pamba Jiji FC
  • Tarehe: 03 Oktoba 2024
  • Uwanja: Azam Complex, Dar es Salaam
  • Muda: Saa 12:30 Jioni (6:30PM EAT)

Fuatilia Hapa

Yanga vs Pamba Jiji Leo 03/10/2024 Saa Ngapi?
Yanga vs Pamba Jiji Leo Saa Ngapi

Timu ya Wananchi, Yanga SC imeanza msimu huu kwa nguvu ya umeme, ikishinda michezo yote mitatu ya awali bila kuruhusu kufungwa goli ata moja. Yanga wamefanikiwa kufunga jumla ya magoli manne katika michezo walocheza hadi sasa na wanapewa nafasi kubwa ya kuendeleza rekodi hiyo bora leo dhidi ya Pamba Jiji. Upande wa Pamba Jiji FC, wamecheza michezo sita hadi sasa na hawajapata ushindi wowote, wakiwa na pointi nne tu kutokana na sare nne, huku wakipoteza michezo miwili.

Kauli za Benchi la Ufundi

Kocha Msaidizi wa Pamba Jiji FC, Henry Mkanwa, amesema kuwa leo watacheza mpira wa kushambulia na kuzuia, huku wakilenga kupata ushindi wao wa kwanza au sare. Hata hivyo, amekiri kuwa wanaingia uwanjani kwa heshima kubwa kwa wapinzani wao, Yanga SC, ambao ni moja ya timu bora zaidi nchini.

“Mpango wetu uko vizuri. Tunakwenda kupambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri. Mungu akijaalia, tunaweza kuondoka na ushindi. Hatuna presha yoyote, tutacheza kwa heshima na kujituma,” alisema Mkanwa.

Kwa upande wa wachezaji, kiungo wa Pamba Jiji, Paulin Kasindi raia wa DR Congo, ameonyesha kujiamini kwao, akieleza kuwa wanajiandaa vema kwa mchezo huo. Kasindi aliongeza kuwa Pamba Jiji hawaji Dar es Salaam kwa kutoa zawadi ya pointi tatu kwa Yanga. Ameahidi kupambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

“Msidhani tunakuja tu kwa ajili ya kuipatia Yanga pointi tatu. Kila mmoja wetu lazima apambanie nafasi yake kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” alisema Kasindi.

Fursa ya Pamba Jiji

Licha ya Pamba Jiji kutopata ushindi katika mechi sita za awali, wachezaji wao wanaonyesha matumaini makubwa kuelekea mchezo huu. Wanaamini kuwa kila timu ina nafasi, na hawataki kuruhusu kushindwa tena. Kiungo Paulin Kasindi alitumia msemo maarufu wa kuwa mshindi wa kweli ni yule anayesimama tena baada ya kuanguka mara nyingi.

“Mshindi wa kweli, akianguka mara tisa, lazima apambane kusimama mara ya kumi,” alisisitiza Kasindi.

Umuhimu wa Mchezo Huu

Kwa Yanga SC, ushindi katika mchezo huu ni muhimu ili kuendelea kujieka katika nafasi nzuri ya kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi na kuendeleza rekodi yao safi huku wakijeweka karibu kulitetea taji lao. Upande wa Pamba Jiji FC, mchezo huu ni fursa kubwa ya kubadili mwelekeo wa msimu wao na kujipatia ushindi wa kwanza ambao utainua ari ya timu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Viingilio Mechi ya Simba Vs Coastal Union 04/10/2024
  2. Ahoua Aingilia Kati Vita ya Assist Ligi Kuu, Awaburuza Feitoto na Aziz Ki
  3. Yanga Yaanza Mkakati wa Kurejea Kileleni mwa Msimamo wa Ligi kuu
  4. Ratiba ya Taifa Stars vs DR Congo Kufuzu AFCON 2025
  5. Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Dhidi ya DR Congo Kufuzu AFCON 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo