Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024 Saa Ngapi?
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), Young Africans SC, leo wanashuka dimbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuwakabili MC Alger ya Algeria. Mchezo huu ni wa mwisho katika hatua ya makundi na una umuhimu mkubwa kwani utaamua hatima ya Yanga kufuzu hatua ya robo fainali. Yanga wanahitaji ushindi wa aina yoyote ili kupata tiketi ya kusonga mbele, huku wapinzani wao MC Alger wakitafuta sare au ushindi ili kujihakikishia nafasi yao.
Taarifa Muhimu za Mechi ya Yanga Vs MC Alger Leo
- Mchezo: Young Africans SC vs MC Alger
- Mashindano: Ligi ya Mabingwa Afrika (TotalEnergies CAFCL)
- Tarehe: 18 Januari 2025
- Uwanja: Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
- Muda: Saa 16:00 (10:00 Jioni)
FUATILIA HAPA Matokeo ya Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024
Hali ya Kundi Kabla ya Mchezo wa Yanga vs MC Alger
Yanga inashikilia nafasi ya tatu katika Kundi lao ikiwa na alama saba, ikitanguliwa na MC Alger wenye alama nane katika nafasi ya pili. Al Hilal tayari wamejihakikishia kufuzu wakiwa kileleni mwa kundi, huku TP Mazembe wakiwa katika nafasi ya mwisho.
Yanga wanapaswa kushinda mchezo wa leo ili kuungana na Al Hilal katika hatua ya robo fainali. Sare au kipigo kwa Yanga kitamaanisha MC Alger wanafuzu na safari ya Yanga itaishia hapa.
Maandalizi ya Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, amesisitiza umuhimu wa mchezo huu na kueleza kuwa timu yake imejiandaa kikamilifu kupata ushindi. Ramovic amesema kuwa morali ya wachezaji iko juu, na mashabiki wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kuipa timu yao nguvu ya kushinda.
“Kila siku malengo yetu ni kushinda, tumejiandaa vizuri na kila mchezaji ana morali ya juu kuhakikisha tunakwenda kutimiza malengo yetu,” alisema Ramovic. Kocha huyo ameongeza kuwa watazingatia nidhamu ya hali ya juu na kutumia mbinu za kiufundi ambazo zitawasaidia kuwadhibiti wapinzani wao.
Nahodha wa Yanga, Dickson Job, pia ameonyesha kujiamini kwa kueleza kuwa wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huu muhimu. Job amesisitiza kuwa kucheza nyumbani mbele ya mashabiki ni faida kubwa, na wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
“Tunatambua umuhimu wa mchezo wa leo. Kumaliza mechi nyumbani ni faida kwetu kwa sababu tunakuwa karibu na mashabiki wetu. Tutapambana kuhakikisha tunashinda mchezo huu kwa sababu kinyume cha hapo tunaondolewa kwenye mashindano,” alisema Job.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ligi 20 Bora Afrika 2025
- Yanga Wamejipanga Kupambana Kesho: Ramovic
- Kocha MC Alger Atamba Kupata Pointi 3 Dhidi ya Yanga Licha ya Joto Kali
- Ligi Kuu Bara Kurejea Februari kwa Moto! Simba na Yanga Kuanza na Viporo
- Mtibwa Sugar Kuwakaribisha Azam FC Manungu kwa Mechi ya Kirafiki
- Ligi Kuu Bara: JKT Tanzania Waitana Kambini, Kocha Apania Maboresho
- Watano Waagwa Azam Fc
- CV ya Jonathan Djogo Kapela: Winga Mpya wa Yanga SC
- Taifa Stars Yapangwa Kundi Laini CHAN 2024
- Makundi ya CHAN 2025 Yatangazwa
Leave a Reply