Yanga Vs CBE SA Leo 21/09/2024 Saa Ngapi

Yanga Vs CBE SA Leo 21/09/2024 Saa Ngapi

Mechi kati ya Yanga SC na CBE SA ya Ethiopia ni miongoni mwa mechi inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania. Leo, tarehe 21 Septemba 2024, timu hizi mbili zitapambana kuisaka tiketi ya kufuzu makundi ya klabu bingwa Afrika katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 2:30 usiku. Mchezo huu ni sehemu ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), ambapo Yanga SC inahitaji matokeo mazuri ili kufuzu hatua ya makundi.

Yanga Vs CBE SA Leo 21/09/2024 Saa Ngapi

Fuatilia Hapa Taarifa Kuhusu Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024

Fuatilia Hapa Matokeo ya Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024

Yanga Inatafuta Ushindi Mkubwa

Yanga SC, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC Tanzania, wataingia kwenye mchezo huu wakiwa na morali kubwa baada ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya CBE kwa bao 1-0 huko Addis Ababa, Ethiopia.

Licha ya ushindi huo, wachezaji wa Yanga na mashabiki walitarajia ushindi wa mabao mengi kutokana na nafasi nyingi walizotengeneza. Hivyo, leo wanatarajia kurudisha heshima yao kwa kushinda kwa idadi kubwa ya mabao.

Dickson Job, nahodha msaidizi wa Yanga, alisema:

“Tulipata ushindi wa bao moja kule Ethiopia, lakini tunajua tulipaswa kushinda kwa mabao mengi zaidi. Hivyo, tumekaa chini na kufanya kazi ya kurekebisha makosa yetu. Leo tunataka kutoa ushindi mkubwa kwa mashabiki wetu.”

Tamko la Wachezaji na Kocha wa Yanga

Wachezaji wa Yanga wamejitolea kuhakikisha wanapata matokeo bora katika mchezo huu wa leo. Kwa mujibu wa Dickson Job, timu hiyo imefanya maandalizi mazuri na inatarajia kushinda kwa kishindo mbele ya mashabiki wao wa Zanzibar.

Kauli ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi:

“Tumejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hii. Tunaheshimu wapinzani wetu, CBE SA, kwani ni timu yenye ubora. Lakini tumejiandaa kuhakikisha hatupi nafasi ya wao kuharibu mpango wetu wa kufuzu. Leo tunahitaji kutumia kila nafasi tunayotengeneza kwa ufanisi.”

Gamondi aliongeza kuwa timu yake imefanya mazoezi ya kutosha, na wamejifunza kutokana na makosa ya mechi ya kwanza. Wachezaji wake wako tayari kutoa ushindi mkubwa nyumbani.

Kwa Nini Hii Mechi ya Yanga vs CBE Ni Muhimu?

Kama Yanga SC itashinda na kufuzu hatua ya makundi, itaweka rekodi ya kufuzu hatua hiyo mara mbili mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Msimu uliopita, Yanga ilifika hadi robo fainali, lakini msimu huu malengo yao ni kufika mbali zaidi.

Wanataka kuonyesha ubora wao kwa kuwapa mashabiki wao ushindi wa kihistoria. CBE SA, licha ya kuwa timu nzuri, inakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya Yanga ambayo imejidhatiti kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.

Saa ya Mechi na Mahali Pa Kutazama

Mashabiki wa Yanga na soka kwa ujumla nchini Tanzania wanatarajia mechi hii kwa hamu kubwa.

Mechi itaanza rasmi saa 2:30 usiku kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Kwa wale ambao hawawezi kufika uwanjani, watakuwa na nafasi ya kuangalia mchezo huo kupitia matangazo ya moja kwa moja yatakayokua yanarushwa na Azam Tv.

Kama wewe ni shabiki wa Yanga au mpenzi wa soka, hakikisha huikosi mechi hii muhimu ambayo itaamua hatma ya mabingwa hao wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Juma Mgunda Anukia KenGold Fc
  2. Yanga Yafika Zanzibar Tayari kwa Mchezo Dhidi ya CBE
  3. NMB Yaungana na Yanga Kuelekea Ligi ya Mabingwa Afrika
  4. Gamondi Aweka Wazi Nia Yake ya Kutwaa Ubingwa wa Afrika
  5. Barcelona Yaanza UEFA Kwa Kichapo cha 2-1 Kutoka kwa Monaco
  6. Manchester City washindwa kutamba dhidi ya Inter
  7. Arsenal Yaambulia Pointi Moja Ugenini, Raya Aokoa Mkwaju wa Penalti
  8. Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo