Yanga Kuwakosa Maxi, Chama na Yao Mechi Dhidi ya TP Mazembe Leo

Yanga Kuwakosa Maxi Chama na Yao Mechi Dhidi ya TP Mazembe Leo

Yanga Kuwakosa Maxi, Chama na Yao Mechi Dhidi ya TP Mazembe Leo

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Clatous Chama, pamoja na beki wa kulia Yao Kouassi na Maxi Nzengeli, wataukosa mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Habari za ndani ya klabu zinasema nyota hao bado hawajawa fiti kwa ajili ya mchezo huu muhimu.

Yanga Kuwakosa Maxi, Chama na Yao Mechi Dhidi ya TP Mazembe Leo

Sababu za Kuukosa Mchezo

Clatous Chama anendelea kuuguza jeraha la mkono, huku Yao Kouassi akiendelea na matibabu ya goti lake. Wachezaji Maxi Nzengeli na Aziz Andambwile, ingawa tayari wameanza mazoezi, hawajafikia viwango vya ushindani vinavyohitajika kwa mechi hii ngumu dhidi ya Mazembe. Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramović, ameweka wazi kuwa kikosi kinachotegemewa kitakuwa na mabadiliko, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na wachezaji walioko tayari kimwili na kiakili.

Hali ya Yanga Katika Kundi A

Kwa sasa, Yanga inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Kundi A ikiwa na pointi moja pekee baada ya michezo mitatu. Timu hiyo ilipoteza michezo miwili na kutoa sare moja.

Msimamo wa Kundi A unavyoonekana kwa sasa:

  1. Al Hilal – Pointi 9
  2. MC Alger – Pointi 4
  3. TP Mazembe – Pointi 2
  4. Yanga – Pointi 1

Kwa matokeo haya, mchezo wa leo ni muhimu sana kwa Yanga ili kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hii mikubwa ya Afrika.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024 Saa Ngapi?
  2. Kikosi cha Kilimanjaro Stars VS Zanzibar Heroes leo 03/01/2024
  3. Viingilio Mechi ya Yanga VS TP Mazembe 04/01/2025
  4. Matokeo ya Zanzibar Heroes VS Kilimanjaro Stars leo 03/01/2024
  5. Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2025
  6. Kikosi Cha Kilimanjaro Stars Kitakacho Shiriki Mapinduzi Cup 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo