Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Tarehe, Matukio na Bei ya Tiketi

Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Sherehe Kubwa ya Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara mara tatu mfululizo Yanga Sc (Timu ya Wananchi), Tarehe Muhimu, Matukio ya Kusisimua, na Bei za Tiketi

Wiki ya Mwananchi, inayojulikana pia kama Yanga Day, ni tukio maalum linalofanyika kila mwaka ili kuadhimisha kilele cha klabu ya Yanga ambapo utambulisho wa kikosi kipya cha wachezaji na benchi la ufundi hufanyika.

Mwaka huu, tukio hili limepangwa kufanyika tarehe 4 Agosti 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam. Hapa chini, tutakupa maelezo yote muhimu kuhusu tarehe, matukio, na bei za tiketi kwa ajili ya Wiki ya Mwananchi 2024.

Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day) Tarehe & Mahali

Tarehe 4 Agosti 2024, katika Uwanja wa kimataifa wa Benjamin Mkapa utakuwa kitovu cha sherehe kuu ya Wananchi ambayo hujulikana kama Yanga Day 2024. Hii ni siku maalum ambapo klabu ya Yanga inakutanisha mashabiki wake kwa shamrashamra za aina yake, huku ikiwatambulisha nyota wapya watakaowakilisha klabu katika msimu ujao.

Utambulisho wa kikosi cha Yanga Sc kuelekea msimu wa 2024/2025 utaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na hatimaye mchezo wa kirafiki ambao utawafanya mashabiki wa Yanga SC kushuhudia kiwango cha kusakata kabumbu kutoka kwa kikosi kipya.

Matukio ya Kutarajia Yanga Day 2024

Wiki ya Mwananchi inajumuisha matukio mbalimbali yenye lengo la kutoa burudani na kuimarisha mshikamano kati ya klabu na mashabiki wake. Baadhi ya matukio yanayotarajiwa ni:

  1. Utambulisho wa Kikosi Kipya: Wachezaji wapya watawasilishwa mbele ya mashabiki kwa mara ya kwanza, wakiwa tayari kuonyesha uwezo wao uwanjani.
  2. Mechi ya Kirafiki: Timu ya Yanga itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu nyingine, ikitumika kama majaribio ya mwisho kabla ya kuanza kwa msimu rasmi.
  3. Burudani kutoka kwa Wasanii: Wasanii mbalimbali watapamba jukwaa, wakitoa burudani ya muziki na ngoma, kuhakikisha mashabiki wanafurahia kila dakika ya sherehe.
  4. Hotuba na Sherehe: Viongozi wa klabu watazungumza na mashabiki, kutoa mipango na malengo ya klabu kwa msimu ujao.

Bei za Tiketi za Wiki ya Mwananchi 2024 na Maeneo ya Kununua

Ili kuhakikisha kila shabiki anapata nafasi ya kushiriki katika sherehe hii, Yanga imeweka viwango tofauti vya tiketi:

  • VIP A: Tsh 50,000
  • VIP B: Tsh 30,000
  • VIP C: Tsh 15,000
  • Jukwaa la Machungwa: Tsh 10,000
  • Mzunguko: Tsh 5,000

Tiketi za Royal

Pia kutakua na tiketi za Royal ambazo zitajumuisha vitu mbalimbali ikiwemo jezi, siti za kukaa VIP A, Huduma ya Chankula, Viburudisho na usafiri wa kwenda na kurudi.Tikite hizi zinapatikana kwa bei ya Tsh 300,000.

Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Tarehe, Matukio na Bei ya Tiketi

Wauzaji wa Tikiti za Yanga Day 2024

Tiketi za Yanga Day 2024 zinapatikana katika maeneo yafuatayo:

  1. Young Africans – Jangwani
  2. Vunja Bei – Kinondoni, Sinza, Mbeya
  3. T-Money Ltd – Kigamboni
  4. Gitano Samweli – Mbagala Zakiem
  5. Khalfan Mohamed – Ilala
  6. Kibacho Juma – Morogoro
  7. Mwanaidi Izina – Morogoro
  8. Godwin Fredy – Geita
  9. Twisty Investment – Geita
  10. Gwambina Lounge – Gwambina
  11. Karoshy Pamba – Dar Live (Zakhiem)
  12. Antonio Service – Sinza, Kivukoni
  13. Tumpe Kamwela – Kigamboni
  14. Sovereign – Kinondoni Makaburini
  15. View Blue Skyline – Mikocheni
  16. Mkaluka Traders – Machinga Complex
  17. New Tech General Traders – Ubungo
  18. Sabana Business – Mbagala Maji Matitu
  19. Juma Burrah – Mbeya
  20. Juma Burrah – Kivukoni
  21. Juma Burrah – Msimbazi
  22. Alphan Hinga – Ubungo
  23. Mtemba Service Co – Temeke
  24. Jackson Kimambo – Ubungo
  25. Shirima Shop – Leaders
  26. Lampard Electronics – DSM

Editor’s Picks:

  1. Kikosi Cha Yanga Vs FC Augsburg Mpumalanga Cup 20/July/2024
  2. Ratiba ya Mpumalanga Premier international Cup 2024
  3. Wachezaji Waliosajiliwa Simba 2024/2025
  4. Rekodi za Simba na Yanga Kufungana
  5. Simba Day 2024: Tarehe Rasmi Yatangazwa na Simba SC
  6. Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji wa Simba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo