Washindi wa Tuzo za MTV VMA 2024

Washindi wa Tuzo za MTV VMA 2024

Washindi wa Tuzo za MTV VMA 2024 | Tuzo za Muziki za MTV VMA

Tuzo za MTV Video Music Awards (VMA) za mwaka 2024 zimefanyika katika ukumbi wa UBS Arena, New York, Septemba 11, 2024.

Hafla hii ya kifahari ilishuhudia mastaa wakubwa wa muziki wakishindania tuzo katika vipengele mbalimbali, huku Taylor Swift na Post Malone wakiongoza orodha ya washindi.

Tuzo hizi zinatambua ubunifu na mafanikio ya wasanii katika tasnia ya muziki ya kimataifa, zikiakisi ushawishi wao kwenye burudani, sanaa, na utamaduni wa pop. Katika makala hii, tutapitia orodha ya washindi wa tuzo za MTV VMA 2024.

Washindi wa Tuzo za MTV VMA 2024

Video Bora ya Mwaka

Kipengele cha Video of the Year kilikuwa kimojawapo cha kipengele chenye ushindani mkubwa, ambapo wasanii mashuhuri kama Ariana Grande, Billie Eilish, na Doja Cat walishindania.

Hata hivyo, Taylor Swift akishirikiana na Post Malone, walijinyakulia ushindi kupitia wimbo wao maarufu, Fortnight. Video hii ilivutia sana kutokana na ubunifu wake, utayarishaji bora, na ushawishi mkubwa kwenye jukwaa la muziki wa pop.

Mshindi: Taylor Swift feat. Post Malone – Fortnight – Republic Records

Washindani wengine waliojumuishwa katika kipengele hiki ni:

  • Ariana Grande – We Can’t Be Friends (Wait for Your Love) – Republic Records
  • Billie Eilish – Lunch – Darkroom / Interscope Records
  • Doja Cat – Paint the Town Red – Kemosabe Records / RCA Records
  • Eminem – Houdini – Shady / Aftermath / Interscope Records
  • SZA – Snooze – Top Dawg Entertainment / RCA Records

Msanii Bora wa Mwaka

Katika kipengele cha Artist of the Year, Taylor Swift aling’ara tena, akiibuka mshindi. Ushindi huu ulikuja baada ya mafanikio yake makubwa kwenye tasnia ya muziki mwaka huu, ambapo alitoa albamu na nyimbo zilizovuma sana.

Mshindi: Taylor Swift – Republic Records

Washindani waliokuwepo ni:

  • Ariana Grande – Republic Records
  • Bad Bunny – Rimas Entertainment
  • Eminem – Shady / Aftermath / Interscope Records
  • Sabrina Carpenter – Island
  • SZA – Top Dawg Entertainment / RCA Records

Wimbo Bora wa Mwaka

Wimbo bora wa mwaka (Song of the Year) ni tuzo inayotambua wimbo ulioathiri sana utamaduni wa muziki kwa mwaka huo. Sabrina Carpenter alishinda kipengele hiki kupitia wimbo wake Espresso, ambao ulikuwa miongoni mwa vibao vinavyopendwa zaidi duniani.

Mshindi: Sabrina Carpenter – Espresso – Island

Washindani wengine ni:

  • Beyoncé – Texas Hold ‘Em – Parkwood Entertainment / Columbia Records
  • Jack Harlow – Lovin on Me – Generation Now / Atlantic Records
  • Kendrick Lamar – Not Like Us – pgLang, Interscope Records
  • Taylor Swift feat. Post Malone – Fortnight – Republic Records
  • Teddy Swims – Lose Control – Warner Records

Msanii Chipukizi Bora

Katika kipengele cha Best New Artist, msanii chipukizi Chappell Roan aliibuka na ushindi. Mafanikio yake yamekuwa ya haraka, na wimbo wake Red Wine Supernova umemjengea umaarufu mkubwa.

Mshindi: Chappell Roan – Island

Washindani wengine walikuwa:

  • Gracie Abrams – Interscope Records
  • Tyla – Epic Records

Ushirikiano Bora

Kwa kipengele cha Best Collaboration, Taylor Swift na Post Malone walishinda kwa mara nyingine kupitia wimbo wao Fortnight, ambao umevuma sana ulimwenguni.

Mshindi: Taylor Swift feat. Post Malone – Fortnight – Republic Records

Washindani waliokuwepo ni:

  • Drake feat. Sexyy Red & SZA – Rich Baby Daddy – OVO / Republic Records
  • GloRilla feat. Megan Thee Stallion – Wanna Be – CMG / Interscope Records
  • Jessie Murph feat. Jelly Roll – Wild Ones – Columbia Records
  • Jung Kook feat. Latto – Seven – BIGHIT MUSIC / Geffen Records
  • Post Malone feat. Morgan Wallen – I Had Some Help – Mercury / Republic / Big Loud

Msanii Bora wa Pop

Katika muziki wa pop, Taylor Swift alishinda tena kupitia kipengele cha Best Pop, akiendelea kuthibitisha uwezo wake wa kuzalisha nyimbo za kuvutia katika aina hii ya muziki.

Mshindi: Taylor Swift – Republic Records

Washindani wengine walikuwa:

  • Camila Cabello – Geffen / Interscope Records
  • Dua Lipa – Warner Records
  • Olivia Rodrigo – Geffen Records
  • Sabrina Carpenter – Island
  • Tate McRae – RCA Records

Msanii Bora wa Hip-Hop

Katika kipengele cha Best Hip-Hop, Eminem alijinyakulia tuzo kwa wimbo wake Houdini, akiwapiku wasanii kama Drake, GloRilla, na Megan Thee Stallion.

Mshindi: Eminem – Houdini – Shady / Aftermath / Interscope Records

Washindani wengine ni:

  • Drake feat. Sexyy Red & SZA – Rich Baby Daddy – OVO / Republic Records
  • GloRilla – Yeah Glo! – CMG / Interscope Records
  • Gunna – Fukumean – Young Stoner Life Records / 300 Entertainment
  • Megan Thee Stallion – BOA – Hot Girl Productions
  • Travis Scott feat. Playboi Carti – FE!N – Cactus Jack / Epic Records

Washindi wa Tuzo Nyingine za MTV VMA 2024

Mwaka huu wa 2024, tuzo za MTV VMA zimetambua mafanikio makubwa katika aina mbalimbali za muziki duniani. Orodha hii inaonyesha baadhi ya washindi katika vipengele vingine:

  • Best R&B: SZA – Snooze – Top Dawg Entertainment / RCA Records
  • Best Rock: Lenny Kravitz – Human – Roxie Records Inc.
  • Best Latin: Anitta – Mil Veces – Floresta Records
  • Best Afrobeats: Tyla – Water – FAX Records / Epic Records
  • Best K-pop: LISA – Rockstar – RCA Records
  • Video for Good: Billie Eilish – What Was I Made For (From Barbie) – Interscope Records
  • Song of Summer: Benson Boone – Beautiful Things – Warner Records

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Washindi wa Ngao ya Jamii Miaka Yote
  2. Washindi wa Tuzo za TFF 2023/2024
  3. Washindi wa Tuzo Dar Port Kagame Cup 2024, Hawa Apa
  4. Washindi wa Tuzo Za ZFF PBZ AWARDS 2024
  5. Washindi Wa Tuzo Za BET 2024
  6. Tuzo za Ligi Kuu England 2023/24: Hawa Apa washindi wa Tuzo EPL
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo