Washindi wa Tuzo za Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025 Mwezi Septemba
Ligi Kuu ya NBC inaendelea kushika kasi, na mwezi Septemba umeshuhudia viwango bora kutoka kwa wachezaji na makocha mbalimbali. Tuzo za Mwezi zimetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutambua wale waliofanya vizuri zaidi. Msimu huu, Fountain Gate wameibuka washindi wakubwa, huku mshambuliaji wao Selemani Mwalimu akijinyakulia tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba.
Mchezaji Bora wa Mwezi, Selemani Mwalimu
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba imekwenda kwa mshambuliaji mahiri wa Fountain Gate, Selemani Mwalimu. Mwalimu ameonyesha kiwango cha juu na mchango mkubwa kwa timu yake, akifunga mabao matatu katika dakika 353 alizocheza. Ufanisi wake uwanjani umesaidia kwa kiasi kikubwa kwa timu ya Fountain Gate kushinda michezo mitatu na kutoka sare moja, huku ikipaa kutoka nafasi ya 15 hadi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu.
Mwalimu aliwashinda wachezaji wengine mahiri walioingia fainali, akiwemo William Edgar (Fountain Gate) na Feisal Saturn (Azam FC). Ushindi huu unadhihirisha ubora wake na uwezo wake wa kuamua matokeo ya mchezo.
Kocha Bora wa Mwezi, Mohamed Muya
Tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi Septemba imekwenda kwa Mohamed Muya wa Fountain Gate. Muya ameiongoza timu yake kwa ustadi mkubwa, akitumia mbinu bora zilizozaa matokeo chanya. Mafanikio ya Fountain Gate mwezi Septemba yanatokana na uongozi wake makini na uwezo wake wa kuhamasisha wachezaji. Muya aliwashinda makocha wazoefu, Rachid Taoussi wa Azam FC na Denis Kitambi wa Singida Black Stars, ambao nao walionyesha uwezo mkubwa mwezi Septemba.
Meneja Bora wa Uwanja, Godwin Israel
Kamati ya Tuzo pia imemtambua Godwin Israel Haquet Omar, Meneja wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, kama Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Septemba. Omar amefanya kazi nzuri katika kuhakikisha uwanja unaendeshwa kwa ubora, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa matukio ya michezo na miundombinu.
Ligi ya Championship:
Katika Ligi ya Championship ya NBC, Raizin Hafidh wa Mtibwa Sugar ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba. Raizin alifunga mabao matatu katika dakika 157, akiiongoza timu yake kushinda michezo yote miwili iliyocheza.
Tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi Septemba katika Ligi ya Championship imekwenda kwa Melis Medo wa Mtibwa Sugar. Medo ameiongoza timu yake kushinda michezo miwili, ikiwa ni pamoja na ushindi wa 2-0 dhidi ya Green Warriors na Cosmopolitan.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Viingilio Mechi ya Simba VS Yanga 19/10/2024
- Fadlu Aanza Mikwara Kuelekea Dabi ya Kariakoo
- Max Nzengeli: “Hakuna Dabi Rahisi Duniani Kote”
- Ratiba ya NBC Championship Tanzania 2024/2025
- Morocco Ahimiza Ubora wa Umaliziaji wa Nafasi Kuelekea Mchezo wa Marudiano na DRC
- Simba Queen na JKT Queens Waanza na Moto Ligi Kuu wanawake
Leave a Reply