Washindi wa Tuzo za CAF 2024 (CAF AWARDS 2024)

Orodha ya washindi wa Tuzo za CAF 2024

Washindi wa Tuzo za CAF 2024 (CAF AWARDS 2024)

Tuzo za CAF za mwaka 2024 zimetolewa usiku wa Jumatatu, Disemba 16, katika hafla kubwa iliyofanyika katikati ya jiji la Marrakech, Nchini Morocco. Hafla hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa soka kutoka bara la Afrika na nje ya Afrika, huku tukio hilo likishuhudiwa na wapenzi wa muziki na michezo. Kwa upande wa Tanzania, Diamond Platnumz aliiwakilisha Tanzania na bongoflavour kama sehemu ya watumbuizaji, akionyesha mchango wake katika kuongeza furaha ya sherehe hii ya kipekee.

Tuzo hizi zilikuwa ni ishara ya ukuaji wa soka barani Afrika, ambapo wachezaji, makocha, na vilabu vilivyofanya vizuri katika mwaka 2024 walitambuliwa kwa mafanikio yao. Miongoni mwa washindi wa tuzo za mwaka huu, mchezaji Ademola Lookman kutoka Nigeria alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa upande wa Wanaume, huku Barbra Banda wa Zambia akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa upande wa Wanawake.

Orodha ya washindi wa Tuzo za CAF 2024

Washindi wa Tuzo za CAF 2024 (CAF AWARDS 2024)

Mchezaji Bora wa Mwaka (Wanaume)

  • Ademola Lookman (Nigeria / Atalanta)

Mchezaji Bora wa Mwaka (Wanawake)

  • Barbra Banda (Zambia / Orlando Pride)

Kipa Bora wa Mwaka (Wanaume)

  • Ronwen Williams (Afrika Kusini / Mamelodi Sundowns)

Kipa Bora wa Mwaka (Wanawake)

  • Chiamaka Nnadozie (Nigeria / Paris FC)

Mchezaji Bora wa Vilabu (Wanaume)

  • Ronwen Williams (Afrika Kusini / Mamelodi Sundowns)

Mchezaji Bora wa Vilabu (Wanawake)

  • Sanaâ Mssoudy (Morocco / AS FAR)

Mchezaji Chipukizi wa Mwaka (Wanaume)

  • Lamine Camara (Senegal / AS Monaco)

Mchezaji Chipukizi wa Mwaka (Wanawake)

  • Doha El Madani (Morocco / AS FAR)

Kocha Bora wa Mwaka (Wanaume)

  • Emerse Fae (Ivory Coast)

Kocha Bora wa Mwaka (Wanawake)

  • Lamia Boumehdi (DR Congo / TP Mazembe)

Timu ya Taifa ya Mwaka (Wanaume)

  • Ivory Coast

Timu ya Taifa ya Mwaka (Wanawake)

  • Nigeria

Klabu Bora ya Mwaka (Wanaume)

  • Al Ahly (Misri)

Klabu Bora ya Mwaka (Wanawake)

  • TP Mazembe (DR Congo)

Bao Bora la Mwaka

  • Mabululu (Angola)

Mwamuzi Bora wa Mwaka (Wanaume)

  • Mutaz Ibrahim (Libya)

Mwamuzi Bora wa Mwaka (Wanawake)

  • Bouchra Karboubi (Morocco)

Msaidizi Bora wa Mwamuzi (Wanaume)

  • Elvis Guy Noupue Nguegoue (Cameroon)

Msaidizi Bora wa Mwamuzi (Wanawake)

  • Diana Chikotesha (Zambia)

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
  2. Kibu Denis Aipa Simba Ushindi Dhidi ya CS Sfaxien Dakika za Jioni
  3. Matokeo ya Simba VS CS Sfaxien Leo 15/12/2024
  4. Simba VS CS Sfaxien Leo 15/12/2024 Saa Ngapi?
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo