Orodha ya Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2025 : Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2025
Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2025
Jeshi la Uhamiaji Tanzania kupitia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji limetangaza orodha rasmi ya waombaji wa nafasi za ajira waliofanikiwa kufuzu hatua za awali na kuteuliwa kuhudhuria usaili. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, jumla ya waombaji 2,115 wamechaguliwa kuhudhuria usaili huo, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 15 Januari, 2025 katika maeneo mawili tofauti kwa waombaji wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Maelekezo ya Mahali na Ratiba za Usaili
Kwa waombaji walioko Tanzania Bara, usaili utafanyika katika:
- Ukumbi wa Maktaba (Library), Ndaki ya Elimu (CoED), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
- Muda wa kuanza: Saa 1:00 asubuhi.
Kwa upande wa waombaji kutoka Zanzibar, usaili utafanyika katika:
- Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Hall, uliopo Tunguu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
- Muda wa kuanza: Saa 1:00 asubuhi.
Waombaji wote wanatakiwa kuheshimu ratiba hii kwa kuhakikisha wanawasili kwa wakati ili kuepuka changamoto zozote zinazoweza kuathiri ushiriki wao katika zoezi hilo muhimu.
Vitu Muhimu vya Kubeba Wakati wa Usaili Wa Jeshi la Uhamiaji
Ili kuhakikisha usaili unafanyika kwa ufanisi, waombaji wote wanapaswa kuwa na vitu vifuatavyo:
- Namba ya Ombi la Ajira (Application ID), iliyotumwa kwao kupitia barua pepe na ujumbe wa simu.
- Kitambulisho chenye picha ya mwombaji, mfano: Kitambulisho cha Taifa, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti au Kitambulisho cha Mkazi au nyaraka nyingine rasmi zinazomtambulisha.
- Kalamu ya wino wa bluu kwa ajili ya matumizi wakati wa usaili.
Maelekezo Maalum kwa Fani za TEHAMA na Ufundi Magari
Waombaji wenye utaalamu katika fani za TEHAMA na ufundi magari wanapaswa kujiandaa kwa ajili ya usaili wa vitendo (Practical Examination). Hii ni hatua muhimu ya kuonyesha ujuzi wao wa kitaalamu kabla ya uteuzi wa mwisho.
Gharama za Chakula, Usafiri, na Malazi
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji amesisitiza kuwa waombaji wote wanapaswa kujigharamia chakula, usafiri, na malazi wakati wote wa kipindi cha usaili. Hii inajumuisha safari ya kwenda na kurudi kutoka katika maeneo yaliyotajwa ya usaili.
Jinsi ya Kupata Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2025
Orodha kamili ya majina ya walioitwa kwenye usaili inapatikana kupitia tovuti rasmi ya Idara ya Uhamiaji:
www.immigration.go.tz
Waombaji wanashauriwa kuingia kwenye tovuti hii ili kuthibitisha majina yao na kujiridhisha na maelekezo yote yaliyotolewa kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye usaili.
Bofya Hapa Kupakua Pdf Yenye Majina Yote
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply