Wachezaji Wapya Yanga (Usajili wa Yanga 2024) | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC, maarufu kama Wanajangwani, imeingia kwenye msimu wa usajili kwa kasi na ari ya aina yake. Katika kuelekea msimu wa 2024/2025, Yanga imepania kufanya kweli na usajili wa wachezaji mahiri ili kuimarisha kikosi chao na kuendeleza utawala wao katika soka la Tanzania. Mashabiki wa Yanga kote nchini wamejaa hamasa na matumaini makubwa kuhusu usajili huu, wakitarajia enzi mpya ya mafanikio makubwa zaidi kwa timu yao pendwa. Makala haya yanakuletea uchambuzi wa kina kuhusu wachezaji wapya waliosajiliwa Yanga, mbinu za uchezaji zitakazotumika, na matarajio ya msimu mpya.
Wachezaji Wapya Yanga | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
Baada ya misimu mitatu ya ubingwa mfululizo, Yanga SC imedhamiria kuendeleza utawala wake katika soka la Tanzania na kuhamishia ubabe huo katika mashindano ya klabu bingwa Afrika. Licha ya kuagana na kocha Nasreddine Nabi, ambaye alikuwa chachu ya mafanikio ya hivi karibuni, Yanga imeendelea kungβara chini ya kocha mpya Miguel Γngel Gamondi.
Ushindi wa kombe la ligi kuu ya NBC na kombe la shirikisho la CRDB, pamoja na kufika robo fainali ya michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25, unathibitisha ubora wa kikosi hiki.
Sasa, Yanga imeweka tarehe moja mwezi wa saba kuwa siku ya kuwatambulisha rasmi wachezaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu wa 2024/2025. Tayari kumekuwa na uvumi kuhusu usajili mkubwa, ikiwemo Clatous Chama kutoka Simba SC na Prince Dube kutoka Azam FC.
Je, uvumi huu utageuka kuwa ukweli? Mashabiki wa Yanga wanasubiri kwa hamu kuona ni nyota gani wapya watakaojiunga na Wanajangwani katika msimu ujao.
1. Clatous Chama
Timu ya Yanga leo tarehe moja mwezi wa Saba imetangaza rasmi Mchezaji Clatous Chama Kujiunga na timu hiyo baada ya tetesi nyingi. Yanga kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram wameandika haya
ππππππ @ClatousCC ni ππππππππππ° Karibu sana Jangwaniππ½
ππππ πππππππππ?#TimuYaWananchi #DaimaMbeleNyumaMwiko pic.twitter.com/vspnJt9QYj
β Young Africans SC (@YoungAfricansSC) July 1, 2024
2. Prince Dube Mpumelelo
Klabu ya Yanga imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo (27) kuwa mchezaji wake mpya kutoka Azam FC kuelekea msimu wa 2024/2025. Mchezaji wa kwanza kutambulishwa kujiunga na Yanga ni kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia kutoka kwa watani wa jadi, Simba SC.
3. Boka Chadrak
Klabu ya Yanga SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili mlinzi mahiri, Boka Chadrak, kutoka FC Saint Eloi Lupopo ya Kinshasa, Congo. Boka, ambaye ni mlinzi wa kushoto, anasifika kwa uwezo wake wa kushambulia na kujilinda kwa haraka, na atakuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu ya Wananchi Yanga sc kwa msimu wa 2024/2025.
4. Khomeini Abubakar
Klabu ya Yanga SC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la shirikisho la CRDB bank, wameendelea kuimarisha kikosi chao kwa kumsajili mlinda mlango chipukizi Aboubakar Khomeini kutoka Singida Black Stars. Usajili huu unaonesha nia ya dhati ya Yanga kuendeleza utawala wao katika soka la Tanzania.
5. Aziz Andabwile
Klabu ya Yanga SC imekamilisha usajili wa kiungo Aziz Andabwile kutoka Fountain Gate FC (Zaman Singida Fountain Gate) kwa mkataba wa miaka miwili. Andabwile mwenye umri wa miaka 24 ametambulishwa leo julai 9 katika kurasa za mitandao ya kijamii za Yanga Sc.
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Matokeo ya Safari Champions vs Yanga Sc Leo 29 June 2024
- Kikosi Cha Yanga 2024/2025 | Wachezaji Wote Wa Yanga
- FIFA Yaiondolea Yanga Adhabu ya Kufungiwa Kusajili
- Wachezaji Wanaolipwa Pesa Nyingi Yanga 2024/2025
- Tetesi za Usajili Yanga: Okrah Kwenye Rada za Kuondoka Yanga? Habari Kamili
- Yanga Yafanikiwa Kutetea Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB 2024
- Picha Za Parade ya Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24
- Yanga SC Kusherehekea Ubingwa wa Ligi kwa Parade Kubwa Mei 25
- Ni Yanga Vs Azam Fainali Ya Kombe La Shirikisho (CRDB Federation Cup)
- Idadi ya Makombe Ya Yanga Ligi Kuu Tanzania
- Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania 2023/24: Ushindi wa Mara ya 30 Kihistoria
Leave a Reply