Vinara wa Assist Ligi Kuu NBC 2023/24: Wafalme wa Pasi za Mwisho Tanzania

Vinara wa Assist Ligi Kuu NBC 2023/24 | Orodha ya Watoa Pasi za Mwisho Ligi Kuu Tanzania 2023/2024

Kama ilivyotarajiwa, msimu wa 2023/24 wa Ligi Kuu ya NBC umeshuhudia wingi wa matukio ya kusisimua. Kuanzia mabao ya kipekee hadi chenga za kuvutia, lakini kilichovutia zaidi ni pasi za mwisho zenye ujuzi mkubwa zilizosababisha magoli mengi muhimu kwa timu mbalimbali. Wakati tunaelekea mwishoni mwa msimu, ni dhahiri utaanza kujiuliza ni mchezaji yupi ambaye ameongoza kwa assists nyingi katika msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania wa 2023/2024?

Huku kila mechi ikiwa ni uwanja wa kushangaza na kila pasi ikiwa ni fursa ya kipekee, jina la mchezaji anayeongoza kwa idadi kubwa ya assists limekuwa likizungumziwa kwa hamu na mashabiki wengi. Majina ya Aziz Ki, Feisal Salum na Clatous Chama yamekuwa yakitajwa sana midomoni mwa mashabiki. Viungo hawa mahiri, wakiwa na uwezo mkubwa wa kuona nafasi na kupiga pasi za maana, wamekuwa injini za timu zao. Lakini je, ni wao pekee waliotawala orodha ya watoa asisti msimu huu?

Tusisahau pia mshangao wa msimu huu: Kipre Junior ambae amekua kiungo mwenye mchango mkubwa Azam. Pia Kouassi Yao kutoka Yanga sc ameonyesha kuwa ubunifu na uwezo wa kupiga pasi za mwisho si dhima ya viungo pekee. Kipaji chake kimekuwa gumzo, na amejihakikishia nafasi miongoni mwa vinara wa pasi za mwisho Tanzania.

Hapa, tumekuletea kwa undani vinara wa assist Ligi Kuu NBC msimu wa 2023/24. Tutaangazia takwimu zao, timu wanazocheza, na nafasi ambazo wanacheza. Jiandae kwa safari ya kusisimua katika ulimwengu wa Wafalme wa Pasi za Mwisho Tanzania.

Vinara wa Assist Ligi Kuu NBC 2023/24

Hawa Ndio Vinara wa Assist Ligi Kuu NBC 2023/24: Wafalme wa Pasi za Mwisho

Nafasi Mchezaji Assists Timu Nafasi Anayocheza
1 Ki Stephane Aziz 8 Young Africans Kiungo
1 Kipre Junior 8 Azam Kiungo
2 Feisal Salum 7 Azam Kiungo
2 Kouassi Yao 7 Young Africans Beki
3 Mohamed Hussein 6 Simba Beki
3 Clatous Chama 6 Simba Kiungo
4 Lusajo Mwaikenda 5 Azam Beki
4 Jackson Mbombo 5 Tabora UTD Kiungo
4 Awesu Awesu 5 KMC Kiungo
4 Clement Mzize 5 Young Africans Mshambuliaji
4 Shomary Rahimu 5 KMC Beki
5 Luis Miquissone 4 Simba Kiungo
5 Pascal Msindo 4 Azam Beki
5 Shomari Kapombe 4 Simba Beki
5 Pacome Zouzoua 4 Young Africans Kiungo
5 Nickson Kibabage 4 Young Africans Beki
5 Ladaki Chasambi 4 Mtibwa Sugar Kiungo
5 Elvis Rupia 4 Singida FG Mshambuliaji
6 Duke Abuya 3 Singida FG Mshambuliaji
6 Obrey Chirwa 3 Kagera Sugar Mshambuliaji
6 Ibrahim Elias 3 KMC Kiungo
6 Joseph Mahundi 3 Ihefu Kiungo
6 Saidi Ntibazonkiza 3 Simba Kiungo
6 Marouf Tchakei 3 Singida FG Kiungo
6 Juma Nyangi 3 Mtibwa Sugar Kiungo
6 Moloko Ducapel 3 Young Africans Kiungo
6 Gibril Sillah 3 Azam Kiungo
6 Mzamiru Yassin 3 Simba Kiungo
6 Jacob Masawe 3 Namungo Kiungo
6 Mudathir Yahya 3 Young Africans Kiungo
6 Mirajy Hassan 3 Coastal Union Beki
6 Kibu Denis 3 Simba Kiungo
7 Bakari Mwamnyeto 2 Young Africans Beki
7 David Luhende 2 Kagera Sugar
7 Ayub Lyanga 2 Azam Mshambuliaji
7 Max Nzengeli 2 Young Africans Kiungo
7 Kelvin Sabato 2 Namungo Mshambuliaji
7 Khalid Aucho 2 Young Africans Kiungo
7 Charles Ilamfia 2 Ihefu Mshambuliaji
7 Adam Adam 2 Mashujaa Mshambuliaji

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Orodha Ya Wafungaji Bora Ligi Kuu Ya NBC Tanzania 2023/2024
  2. Vinara wa Clean Sheets Ligi Kuu NBC Premier League 2023/2024
  3. Msimamo wa Ligi Kuu ya Zanzibar 2023/2024 PBZ Premier League Table
  4. Msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
  5. Msimamo Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga 2023/24
  6. Msimamo wa Ligi Kuu Hispania La Liga 2023/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo