Viingilio Yanga Vs Simba Vita ya Ngao Ya Jamii 2024
Ngao ya Jamii ni moja kati ya michuano inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka Tanzania. Mechi hizi hutoa fursa ya kipekee kwa timu bora zaidi nchini kuonyesha ubabe wao kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mwaka huu, vita ya titani itashuhudiwa tena kati ya watani wa jadi, Yanga SC na Simba SC, itakayofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Hii ni mechi inayovuta hisia za mashabiki wengi kutokana na ushindani wa jadi kati ya klabu hizi mbili kubwa nchini.
Ratiba ya Michuano ya Ngao ya Jamii 2024
Michuano ya Ngao ya Jamii 2024 itaanza rasmi tarehe 8 Agosti, ambapo Azam FC watakutana na Coastal Union katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 10:00 jioni. Mechi inayosubiriwa zaidi ni ile kati ya Simba SC na Yanga SC, ambayo itapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.
Mechi zote za mwisho zitachezwa tarehe 11 Agosti, ambapo mechi ya kusaka mshindi wa tatu itaanza saa 9:00 alasiri na fainali kuchezwa saa 1:00 usiku. Mfumo wa timu nne katika Ngao ya Jamii ulianza rasmi msimu uliopita, na bingwa wa Ligi Kuu kucheza na mshindi wa tatu, huku mshindi wa pili akimenyana na mshindi wa nne.
Viingilio vya Mechi ya Ngao ya Jamii 2024
Mashabiki wanapaswa kujipanga mapema ili kuweza kushuhudia mechi hizi za ngao ya jamii. Viingilio rasmi kwa mechi kati ya Yanga SC na Simba SC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ni kama ifuatavyo:
- Mzunguko: TSH 5,000
- Machungwa: TSH 10,000
- VIP C: TSH 20,000
- VIP B: TSH 30,000
- VIP A: TSH 50,000
Viingilio hivi vimetangazwa mapema ili kuwapa mashabiki nafasi ya kupanga bajeti zao na kuhakikisha wanapata nafasi ya kushuhudia moja kwa moja pambano hili kubwa linalovuta hisia za wengi.
Maandalizi ya Timu
Yanga SC na Simba SC, zote zikiwa na historia ndefu na mafanikio makubwa katika soka la Tanzania, zimekuwa zikijiandaa kwa mechi hii kwa maandalizi ya hali ya juu. Simba SC walikuwa mabingwa wa msimu uliopita baada ya kuifunga Yanga SC kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90. Azam FC walimaliza nafasi ya tatu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Ngao ya Jamii 2024
- Matokeo ya Yanga Vs Red Arrows Leo Agosti 03 2024 – Yanga Day
- Matokeo ya Simba Vs APR Leo 03 Agosti 2024 – Simba Day
- Kikosi Cha Simba 2024/2025 | Wachezaji Wote wa Simba
- Orodha ya Makocha Timu za Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
- Kamati Mpya Ya Mashindano Simba Sc 2024/2025 Yatangazwa
Leave a Reply