Viingilio Mechi ya Tabora united Vs Yanga SC Leo 02/04/2025

Viingilio Mechi ya Tabora united Vs Yanga SC Leo 02 04 2025

Viingilio Mechi ya Tabora united Vs Yanga SC Leo 02/04/2025

Tabora United leo itawakaribisha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, katika dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora, kwa mchezo wa kusisimua wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025. Mechi hii inatajwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia ya timu hizi msimu huu, ambapo katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Tabora iliishangaza Yanga kwa kuichapa 3-1 jijini Dar es Salaam.

Tiketi na Viingilio Mechi ya Tabora united Vs Yanga SC Leo 02/04/2025

Kwa mashabiki wanaotaka kushuhudia mtanange huu moja kwa moja uwanjani, tiketi zinapatikana kwa viwango vifuatavyo:

  • VIP: TSH 15,000/=
  • Mzunguko: TSH 5,000/=

Tiketi zinapatikana katika vituo vifuatavyo:

  • TTCL – Makao Makuu
  • Nana Home Decoration (Uhazili)
  • Mango Spare – Stendi Mpya ya Mabasi
  • Rama Pay Point – Chuo cha Utumishi wa Umma (Uhazili)
  • Kumbi za mpira za Big Brother (Madaraka Road)

Viingilio Mechi ya Tabora united Vs Yanga SC Leo 02/04/2025

Uchambuzi wa Mechi

Mchezo wa leo unazikutanisha timu mbili zenye dhamira tofauti lakini zenye kiu ya alama tatu. Yanga SC, inayonolewa na kocha Miloud Hamid, inaingia dimbani ikiwa na rekodi ya kushinda mechi nne kati ya tano zilizopita za ligi, huku ikifunga jumla ya mabao 16, ikimaanisha wastani wa mabao matatu kwa kila mchezo.

Kwa upande wa Tabora United, ambayo kwa sasa inanolewa na kocha mpya, Genesis Mang’ombe kutoka Zimbabwe, inajitahidi kujiweka katika nafasi bora kwenye msimamo wa ligi.

Timu hii inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 37, huku ikiwania kupanda hadi nafasi ya nne kwa ushindi wa leo. Hata hivyo, changamoto kubwa kwa Tabora United ni safu yake ya ulinzi, ambayo imeruhusu mabao 28 katika michezo 23 msimu huu.

Kwa Yanga, ushindi wa leo utaiweka katika nafasi nzuri zaidi kwenye mbio za ubingwa, kwani kwa sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 58. Ikiibuka na ushindi, itafikisha alama 61 na kujitanua zaidi kileleni.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tabora United VS Yanga Leo 02/04/2025 Saa Ngapi?
  2. Real Madrid Yaweka Dau la Pauni Milioni 90 Kumnasa Bruno Fernandez
  3. Kagera Sugar Yagonga Mwamba Usajili wa George Mpole
  4. Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la FA 2024/2025 England
  5. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza 2024/2025
  6. Haaland na Marmoush Waipeleka Man City Nusu Fainali FA Cup
  7. Nyota Wa Real madrid Hatiani Kuikosa Robo fainali UEFA Dhidi ya Arsenal
  8. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo