Viingilio Mechi ya Simba VS Yanga 19/10/2024 | Vituo vya Kukata Tikezi za Simba Sc Vs Yanga
Mechi ya Kariakoo Derby kati ya Simba SC na Yanga SC, ambayo ni moja ya michezo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Tanzania, itafanyika Jumamosi, Oktoba 19, 2024. Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 11:00 jioni. Simba SC, ambao ni wenyeji wa mchezo huo, wametangaza rasmi viingilio vya mechi hii kupitia Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally.
Viingilio Mechi ya Simba VS Yanga 19/10/2024
Kwa mujibu wa tangazo rasmi la klabu ya Simba, viingilio vya mchezo vimepangwa kwa viwango tofauti, ili kuwapa mashabiki wote nafasi ya kuhudhuria: Kiingilio cha chini zaidi kikiwa ni Tsh 5,000 kwa mashabiki wa kawaida na cha bei ya juuu kikiwa ni Tsh 50,000.
- VIP A: Tsh 50,000
- VIP B: Tsh 30,000
- VIP C: Tsh 20,000
- Orange: Tsh 10,000
- Mzunguko: Tsh 5,000
Ahmed Ally amesisitiza kuwa mashabiki wa Simba wanatakiwa kununua tiketi zao mapema, kutokana na ukweli kwamba Simba ndio wenyeji wa mchezo huo, na tiketi zinatarajiwa kuisha haraka kutokana na idadi kubwa ya mashabiki.
Wapi Kununua Tiketi?
Kwa wale wanaotaka kupata tiketi zao kwa njia rahisi, Simba SC imeweka vituo mbalimbali vya kuuza tiketi ili kuhakikisha mashabiki wanapata huduma bora. Tiketi zinapatikana kwenye vituo mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine yaliyo karibu. Baadhi ya vituo hivyo ni pamoja na:
- Lampard Electronics – Simba HQ, Msimbazi
- Vunja Bei Shops – Maduka yote (Dar es Salaam)
- New Tech General Traders – Yenu Bar
- Sabana Business Center – Mbagala Maji Matitu
- TTCL Shops – Dar es Salaam
- Juma Burrah – Msimbazi Center
- Halphani Hingaa – Oilcom Ubungo
- Mtemba Service Company – Temeke
- Jackson Kimambo – Ubungo Rombo
- Mkaluka Traders Ltd – Machinga Complex
- Khalfani Mohammed – Ilala Bungoni
- Karoshy Pamba Collection – Dar Live
- Gisela Shirima – Dahomey Street
- Gwambina Lounge – Temeke Opp Duce
- Antonio Service Co. – Sinza na Kivukoni
- Tumpe Kamwela – Kigamboni
- Sovereign Co. – Kinondoni Makaburini
Njia Mbadala za Kununua Tiketi
Pamoja na vituo hivyo, mashabiki wanaweza pia kununua tiketi kwa urahisi kupitia mitandao ya simu, ikiwa ni njia rahisi na ya haraka kwa wale ambao hawana nafasi ya kufika kwenye vituo vya tiketi. Ahmed Ally amewataka mashabiki kuwasili mapema uwanjani ili kuepuka msongamano wa dakika za mwisho na kuhakikisha wanaingia kwa utaratibu mzuri. Lango litafunguliwa mapema ili kuwapa mashabiki nafasi ya kufurahia burudani ya awali kabla ya mechi kuanza saa 11:00 jioni.
Mapendekezo ya Mhariri;
- Fadlu Aanza Mikwara Kuelekea Dabi ya Kariakoo
- Max Nzengeli: “Hakuna Dabi Rahisi Duniani Kote”
- Ratiba ya NBC Championship Tanzania 2024/2025
- Morocco Ahimiza Ubora wa Umaliziaji wa Nafasi Kuelekea Mchezo wa Marudiano na DRC
- Simba Queen na JKT Queens Waanza na Moto Ligi Kuu wanawake
- Pamba Jiji FC Yafanya Vikao Vizito Baada ya Mwanzo Mbovu Ligi Kuu
Leave a Reply