Viingilio Mechi ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025
Vinara wa ligi kuu ya NBC Tanzania na mabingwa watetezi Yanga SC, leo wanatarajiwa kukipiga dhidi ya wajelajela JKT Tanzania katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni jijini Dar Es Salaam. Mchezo huu wa mzunguko wa pili wa ligi unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa, huku timu zote zikiwa na lengo la kupata pointi muhimu kwa msimu huu wa 2024/2025.
Kwa Yanga SC, ushindi ni muhimu ili kuimarisha nafasi yao ya kwanza kwenye msimamo wa ligi na kuweka msingi mzuri wa kutwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo. Hadi sasa, Yanga wamecheza michezo 17 na kujikusanyia pointi 45, wakiwa wamepata ushindi mara 15 na kupoteza michezo miwili pekee. Wapinzani wao wa karibu, Simba SC, wana pointi 44, hali inayoleta ushindani mkali kwenye nafasi ya juu ya msimamo wa ligi.
Kwa upande wa JKT Tanzania, licha ya changamoto msimu huu, wamefanikiwa kufikisha pointi 19 kwenye michezo 17. Wanatarajia kutumia faida ya kucheza nyumbani kuhakikisha wanapata matokeo mazuri dhidi ya mabingwa watetezi. JKT wameonyesha uwezo wa kulinda uwanja wao wa nyumbani msimu huu, hali inayoweza kuwapa matumaini ya kuibuka na ushindi au angalau pointi moja.
Viingilio na Vituo vya Tiketi Za Mechi ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo
Mashabiki wanaotarajiwa kuhudhuria mchezo huu watahitaji kujipanga mapema kwa viingilio ambavyo vimegawanywa katika madaraja mawili:
- Mzunguko: TSH 10,000/=
- VIP: TSH 20,000/=
Tiketi za mchezo huu zinapatikana katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam, vikiwemo:
- Mbuyuni JKT Pharmacy (Sinza)
- Vunjabei Shops (Kinondoni)
- Gitano Samweli (Mbagala Zakhiem)
- Lampard Electronics (Kariakoo)
- Karoshy Pamba Kali (Dar Live, Mbagala)
- Khalfani Mohammed (Ilala)
- Jackson Kimambo (Ubungo Kibo)
- Gisela Shirima (Dahomey St/Kinondoni)
- Suma JKT (Mwenge)
- T-Money Agent (Kigamboni)
- Perfect Decision Stationary (Boko Magengeni)
Mashabiki wanashauriwa kununua tiketi mapema ili kuepuka msongamano siku ya mechi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025
- Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 10/02/2025
- Bao la Kaseke Laipa Pamba Ushindi Dhidi ya Azam FC
- Ushindi Dhidi ya Dodoma Jiji Wampa Jeuri Minziro
- Ngassa: Mechi dhidi ya Simba itakuwa ngumu, lakini tunajua pakupenya
- KenGold Yaahidi Kujifuta Machozi ya 6-1 Mbele ya Fountain Gate
- Ratiba ya Mechi za Tanzania (Taifa Stars) Afcon 2025
- CAF Yatangaza Ratiba Ya Fainali za Afcon 2025
- Droo ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025 Hatua ya 32 & 16 Bora
- Matokeo ya Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
- Kikosi cha Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
- CV ya Miloud Hamdi, Kocha Mpya wa Yanga 2025
Leave a Reply