Usajili Watainiwa Kidato Cha Sita 2025 Kuanzia 01 Julai 2024

Usajili Watainiwa Kidato Cha Sita 2025 Kuanzia 01 Julai

Kama wewe ni miongoni mwa wahitimu wa kidato cha sita ambao walishindwa kupata matokeo mazuri katika mtihani wa taifa wa kidato cha sita na kushindwa kuendelea na masomo ya vyuo vikuu basi hapa tumekuletea habari njema. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetoa taarifa muhimu kuhusu usajili wa wanafunzi watakaofanya mtihani wa kidato cha sita (ACSEE) mwaka 2025.

Nafasi hii ya upendeleo wa kurudia kunya mtihani wa kidato cha sita hutolewa na NECTA kila mwaka ambapo baraza la mitihani huandaa usajili kwa watahiniwa wa kujitegemea wanaotarajia kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE). Kwa mwaka 2025, usajili huo utaanza rasmi tarehe 01 Julai 2024. Katika chapisho hili, tumekuletea maelezo ya kina kuhusu mchakato wa usajili, hatua za kufuata, na taratibu muhimu za kuhakikisha usajili wako unakamilika kwa ufanisi.

Usajili Watainiwa Kidato Cha Sita 2025 Kuanzia 01 Julai 2024

Nani Anaweza Kujisajili?

Usajili huu ni kwa wale wote ambao wanampango na wamekidhi vigezo vya kufanya mtihani kama “watahiniwa wa kujitegemea.” Hii ina maana kwamba mtahiniwa hajasajiliwa na shule yoyote na atafanya mtihani kama mwanafunzi wa kujitegemea.

Kipindi cha Usajili na Ada

Kwa watahiniwa wa kujitegemea wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Sita 2025, usajili umegawanywa katika vipindi viwili:

  • Usajili wa Kawaida: Kuanzia tarehe 01 Julai hadi 30 Septemba 2024, ada ya usajili itakuwa Shilingi 50,000/=.
  • Usajili wa Kuchelewa: Kuanzia tarehe 01 Oktoba hadi 31 Oktoba 2024, ada ya usajili itakuwa Shilingi 65,000/=. Ni muhimu kufahamu kwamba hakutakuwa na usajili wowote baada ya tarehe 31 Oktoba 2024.

Utaratibu wa Usajili Watainiwa Kidato Cha Sita 2025

Usajili wa watahiniwa wakujitegemea utafanyika kwa njia ya mtandao (online) kupitia tovuti ya NECTA (www.necta.go.tz). Kabla ya kuanza mchakato wa usajili, watahiniwa wanapaswa kufuata hatua zifuatazo:

  1. Kupata Namba Rejea (Reference Number): Watahiniwa wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani vilivyoidhinishwa ili kuchukua Namba Rejea. Namba hizi hutolewa bure.
  2. Malipo ya Ada: Baada ya kupata Namba Rejea, watahiniwa watahitaji kufanya malipo ya ada kupitia Benki kwa kutumia ‘Control Number’ itakayotolewa.

Jinsi ya Kujisajili kama Mtahiniwa wakujitegemea Kwenye Mtihani wa Kidato cha Sita 2025

Mchakato wa kujisajili katika mtihani wa kidato cha sita 2025 kama mtahiniwa wa kujitegemea ni rahisi na umewekwa kuwa wa mtandaoni ili kurahisisha mambo. Lakini kabla ya kuanza mchakato huo, hakikisha una namba rejea na namba ya malipo (control number) kutoka benki. Fuata hatua hizi ili kuhakikisha usajili wako unafanikiwa:

  1. Tembelea Tovuti ya NECTA: Fungua tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania kupitia www.necta.go.tz.
  2. Fuata Maelekezo ya Kujisajili: Tovuti itatoa maelekezo ya hatua kwa hatua kuhusu jinsi ya kutengeneza ‘Control Number’ na jinsi ya kujisajili.
  3. Lipa Ada ya Usajili: Fanya malipo ya ada kupitia benki kwa kutumia ‘Control Number’ iliyotolewa.
  4. Kamilisha Usajili: Baada ya kufanya malipo, endelea na hatua za mwisho za kujisajili kupitia mfumo wa mtandao wa NECTA.

Watahiniwa wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza mwishoni mwa kipindi cha usajili. Mfumo wa usajili utafungwa moja kwa moja baada ya tarehe ya mwisho ya usajili kukamilika, hivyo ni muhimu kufuata ratiba iliyopangwa. Kwa ufafanuzi zaidi na msaada wa kiufundi, watahiniwa wanaweza kuwasiliana na Wakuu wa Vituo vya Mitihani vya Watahiniwa wa Kujitegemea au kutembelea tovuti ya NECTA kwa taarifa zaidi.

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Mitihani Ya NECTA Kidato Cha Nne Pdf Download
  2. Matokeo ya kidato cha sita 2024 Yanatoka Lini?
  3. Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2024
  4. Nafasi Mpya Za Kazi Chuo Kikuu cha SUA: Mwisho wa Kutuma Maombi ni 19 Mei 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo