Usaili Jeshi la Zimamoto 2025 Kuanza Aprili 5 – 17, 2025
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF. John W. Masunga, ametangaza rasmi kuwa usaili wa vijana waliotuma maombi ya ajira kupitia mfumo wa ZIMAMOTO RECRUITMENT (ajira.zimamoto.go.tz) utafanyika kuanzia tarehe 05 Aprili, 2025 hadi tarehe 17 Aprili, 2025. Usaili utaanza saa 1:00 asubuhi kwa kila kundi, hivyo waombaji wanahimizwa kufika kwa wakati.
Ratiba ya Usaili Jeshi la Zimamoto kwa Makundi Mbalimbali
Waombaji wa Elimu ya Kidato cha Nne:
Usaili wao utaanza tarehe 05 Aprili, 2025 na kumalizika tarehe 09 Aprili, 2025. Kila mshiriki atahitajika kuhudhuria usaili katika mkoa aliouchagua wakati wa kutuma maombi.
Waombaji Wenye Shahada na Taaluma Mbalimbali:
Usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 14 Aprili, 2025 hadi tarehe 17 Aprili, 2025. Usaili wa Mahojiano utafanyika katika Ukumbi wa Andengenye – Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Dodoma.
Maelekezo Muhimu kwa Walioitwa kwenye Usaili Jeshi la Zimamoto
Ili kuhakikisha usaili unafanyika kwa ufanisi, waombaji wote wanapaswa kuzingatia masharti yafuatayo:
- Kila mshiriki ahudhurie kwa tarehe aliyopewa, kwani kutokuhudhuria kwa wakati kutasababisha kuondolewa kwenye mchakato wa usaili.
- Mavazi ya staha na nadhifu yanahitajika kwa washiriki wote.
- Kila mshiriki ajihadharishe na matapeli, kwani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji halihusishi ada yoyote kwenye mchakato huu.
Nyaraka Muhimu za Kubeba
Waombaji wote wanapaswa kuwasilisha nyaraka halisi zilizotumika kwenye maombi yao. Hizi ni pamoja na:
- Cheti cha Kidato cha Nne au Kidato cha Sita
- Vyeti vya taaluma husika kwa waombaji wa shahada na fani nyingine
- Cheti cha kuzaliwa
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA
- Leseni halisi ya Udereva (Daraja E) kwa waombaji wa nafasi ya Udereva
Gharama za Usaili
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji halitatoa malipo ya usafiri, chakula, au malazi kwa waombaji. Kila mshiriki anatakiwa kugharamia mahitaji yake binafsi kwa kipindi chote cha usaili.
Tahadhari kwa Washiriki
Waombaji wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanahudhuria usaili katika tarehe zao maalum. Mtu yeyote atakayefika siku ambayo si ya usaili wake hatapokelewa. Kwa maelezo zaidi, waombaji wanashauriwa kutembelea tovuti rasmi ya ajira.zimamoto.go.tz ili kupata taarifa sahihi na rasmi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Majina Ya WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji 2025
- Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Polisi 2025
- Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA 2025 pdf
- Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Polisi 2025
- Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya Jeshi la Polisi Tanzania 2025
- Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA Kutangazwa Machi 22, 2025
- Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili MDAs NA LGAs 2025
- Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs NA LGAs 2025
- Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC 2025 Mkoa wa Dar es Salaam
Leave a Reply