Ubora wa Dube na Pacome Wamfanya Kocha CBE Kuingiwa na Hofu

Ubora wa Dube na Pacome Wamfanya Kocha CBE Kuingiwa na Hofu

Yanga SC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wametua jijini Addis Ababa, Ethiopia, wakiwa na ari ya kuendeleza wimbi lao la ushindi katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Hata hivyo, kocha wa wenyeji, Sisay Kebede wa CBE SA, hajapuuza ubora wa Yanga, haswa akisisitiza uwezo wa kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua na mshambuliaji hatari Prince Dube.

Katika mahojiano ya hivi karibuni, kocha Kebede alikiri kuwa safu ya kiungo ya Yanga, inayoongozwa na Pacome, Chama, Nzengeli, na Aziz Ki, inatisha kwa uwezo wao wa kucheza soka la kisasa, kasi, na uwezo wa kupokonya mpira kwa urahisi. Aidha, safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Dube, ambaye tayari ameshafunga mabao matatu msimu huu, inazidi kuongeza presha kwa wenyeji.

Yanga wameanza msimu huu kwa kishindo, wakifunga jumla ya mabao 17 katika mechi tano za mashindano, huku wakiruhusu bao moja tu. Mbali na Dube, wachezaji wengine kama Aziz Ki, Clement Mzize, na Maxi Nzengeli wamekuwa na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji. Kipa Djigui Diarra amekuwa nguzo imara langoni, akiondoka na ‘cleansheet’ nne katika mechi hizo tano.

Ubora wa Dube na Pacome Wamfanya Kocha CBE Kuingiwa na Hofu

Rekodi Nzuri ya Yanga Afrika Yazidi Kuwatia Presha CBE

Kocha Kebede pia alikiri kuwa rekodi ya Yanga katika mashindano ya Afrika, ikiwa ni pamoja na kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023, inawafanya kuwa timu ya kuogopwa.

Yanga Yajipanga Vyema Licha ya Changamoto

Licha ya kukabiliwa na changamoto ya kuwakosa wachezaji wawili muhimu, Nickson Kibabage na Farid Mussa, Yanga wametua Ethiopia wakiwa na kikosi kamili cha wachezaji 25, wakiwa tayari kwa mtanange huo utakaofanyika Jumamosi saa 9 alasiri.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Goli Pekee la Ngushi Laipa Mashaujaa Ushindi Dhidi ya Coastal Union
  2. Nani Atashinda Ballon d’Or 2024? Rodri, Vinicius Jr, Au Jude Bellingham?
  3. Yanga Vs CBE SA: Saa Ngapi Mechi Inaanza?
  4. Lawi Ndani ya Kikosi cha Coastal Union Dhidi ya Mashujaa
  5. Kocha wa Kagera Sugar Aelezea Masikitiko Baada ya Vipigo Mfululu
  6. Wachezaji Simba Waahidi Ushindi Dhidi ya Al Ahly Tripoli
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo