Twiga Stars Yavuka Raundi ya Pili WAFCON Baada ya Sare Dhidi ya Guinea

Twiga Stars Yavuka Raundi ya Pili WAFCON Baada ya Sare Dhidi ya Guinea

Twiga Stars Yavuka Raundi ya Pili WAFCON Baada ya Sare Dhidi ya Guinea

Timu ya Taifa ya wanawake, Twiga Stars, imefanikiwa kuvuka raundi ya pili ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Guinea ya Ikweta katika mchezo wa marudiano. Ushindi wa jumla wa mabao 4-2 umewapa nafasi ya kusonga mbele katika safari yao ya kuelekea fainali zitakazofanyika Morocco mwaka 2026.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Twiga Stars ilipata ushindi wa mabao 3-1 kwa goli kutoka kwa Stumai Abdallah, Enekia Lunyamila, na Diana Msewa. Licha ya changamoto walizokutana nazo ugenini, Twiga Stars walionyesha uimara na kupambana kwa kiwango cha juu kuhakikisha wanapata matokeo ya kuridhisha.

Ufanisi wa Twiga Stars unatokana na ubora wa kikosi chao, ambacho kinajumuisha wachezaji waliobobea katika ligi za ndani na nje ya nchi. Wachezaji kama Clara Luvanga (Al Nassr), Enekia Lunyamila (Mazaltan), na Diana Msewa (Trabzonspor, Uturuki) wameonyesha uwezo wa hali ya juu. Aidha, nyota kama Stumai Abdallah, Donisia Minja, Naijat Abbas (JKT Queens), na Aisha Mnunka (Simba Queens) walichangia mafanikio ya timu.

Twiga Stars Yavuka Raundi ya Pili WAFCON Baada ya Sare Dhidi ya Guinea

Mafanikio haya yamechangiwa na viwango vya juu vya wachezaji hawa, ambapo Clara Luvanga anaongoza kwa mabao 12 katika ligi ya Saudi Arabia, huku Stumai akiwa kinara wa mabao Ligi Kuu ya Tanzania akiwa na mabao 18. Kwa upande wa ulinzi, Naijat Abbas ameongoza kwa clean sheets nane, jambo linalodhihirisha uimara wa safu ya ulinzi ya Twiga Stars.

Katika mechi zote mbili, Twiga Stars walionyesha ari kubwa ya kupambana. Katika mchezo wa kwanza, licha ya kuwa nyuma kwa bao 1-0 kipindi cha kwanza, walirejea kwa kasi na kushinda 3-1. Hali kama hiyo ilijitokeza katika mchezo wa marudiano, ambapo walifungwa kipindi cha kwanza lakini walirejea kwa nguvu na kufunga bao la kusawazisha kupitia Enekia Kasongo.

Uwezo huu wa kupambana hadi dakika ya mwisho unaonyesha dhamira ya timu kuhakikisha wanapata nafasi ya kufuzu WAFCON. Safu ya ulinzi ya Twiga Stars imeonekana kuwa imara, huku washambuliaji wao wakionyesha uwezo mkubwa wa kumalizia nafasi.

Hatua Inayofuata: Kukabiliana na Ethiopia

Baada ya kuvuka hatua hii, sasa Twiga Stars watakutana na Ethiopia katika raundi ya pili ya kufuzu. Ethiopia ni timu yenye rekodi nzuri katika ukanda wa Afrika Mashariki, ikiwa na safu imara ya ushambuliaji inayoongozwa na Loza Abera wa DC Power FC, Marekani.

Mechi ya kwanza itapigwa Oktoba 20 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, na Twiga Stars wanapaswa kupata ushindi mzuri nyumbani ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kufuzu. Historia inaonyesha kuwa Tanzania na Ethiopia zimekutana mara saba, ambapo Tanzania imeshinda mara moja, Ethiopia mara tatu, huku mechi mbili zikiisha kwa sare. Hii inamaanisha kuwa Twiga Stars wanahitaji maandalizi mazuri kuhakikisha wanapata ushindi wa kihistoria.

Timu Zilizofuzu na Ratiba ya Mechi Zijazo

Mbali na Tanzania, Kenya nayo imefanikiwa kufuzu kwa kuitoa Tunisia na sasa itapambana na Gambia. Nyingine zilizoingia raundi ya pili ni pamoja na Angola, Malawi, Botswana, Afrika Kusini, Namibia, Zambia, Burundi, Burkina Faso, Algeria, Cameroon, Misri, Ghana, Benin, Nigeria, Guinea, Mali, Senegal, na Ivory Coast. Mechi za raundi ya pili zitachezwa kuanzia Oktoba 20 hadi 28 mwaka huu.

Twiga Stars wanaendelea kuonyesha maendeleo makubwa kwenye soka la wanawake na wana nafasi kubwa ya kufuzu kwa fainali za WAFCON ikiwa wataendelea na juhudi zao za kupambana uwanjani. Tanzania sasa inasubiri mtihani mgumu dhidi ya Ethiopia, huku matumaini yakiwa juu kwa mashabiki wa soka nchini.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Antony Afutiwa Kadi Nyekundu, Sasa Ruksa Kuivaa Madrid
  2. Matokeo ya Equatorial Guinea vs Twiga Star Leo 26/02/2024
  3. Man United Wamnyemelea Xavi Kuchukua Mikoba ya Amorim
  4. Kocha Melis Medo Atua Singida Black Stars Kama Kocha Msaidizi
  5. Simba yajikuta Pabaya Baada ya Sare ya 2-2 Dhidi ya Azam
  6. Washindi wa Tuzo za Wachekeshaji Tanzania 2025
  7. Hiki Apa Kikosi cha Simba vs Azam Fc Leo 24/02/2025
  8. Matokeo ya Simba vs Azam Fc Leo 24/02/2025
  9. Matokeo ya Mashujaa VS Yanga Sc Leo 23/02/2025
  10. Kikosi cha Yanga vs Mashujaa Leo 23/02/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo