Trippier Atangaza Kustaafu Soka La Kimataifa

Trippier Atangaza Kustaafu Soka La Kimataifa

Trippier Atangaza Kustaafu Soka La Kimataifa

Kieran Trippier, beki wa kulia wa Newcastle United na mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya England, ametangaza kustaafu soka la kimataifa akiwa na umri wa miaka 33. Trippier, ambaye ameichezea England mara 54, amekuwa mchezaji tegemeo kwa timu hiyo tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017 chini ya kocha Gareth Southgate.

Trippier Atangaza Kustaafu Soka La Kimataifa

Safari ya Trippier Katika Timu ya Taifa

Katika kipindi cha miaka saba, Trippier amekuwa mchezaji muhimu katika safu ya ulinzi ya England, akitoa mchango mkubwa katika mashindano makubwa manne aliyoshiriki. Alifunga bao lake pekee la kimataifa dhidi ya Croatia katika nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2018, bao lililokumbukwa sana na mashabiki wa England.

Trippier pia aliongoza England kama nahodha katika mechi tatu, jambo ambalo ni heshima kubwa kwa mchezaji yeyote. Katika mashindano ya Euro 2024, alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza mechi sita za mwanzo kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Luke Shaw katika fainali.

Ujumbe wa Kuaga wa Trippier

Kupitia ujumbe aliouweka kwenye mitandao ya kijamii, Trippier alielezea furaha yake na heshima aliyopata kwa kuwakilisha taifa lake. “Sikuwahi kufikiria kama kijana mdogo kutoka Bury ningeweza kuchezea nchi yangu, achilia mbali kufikisha michezo 54,” alisema Trippier.

Aliendelea kwa kutoa shukrani zake kwa kocha Gareth Southgate na benchi la ufundi kwa kumwamini na kumpa nafasi katika kikosi cha England. “Nimekuwa na fursa ya kushiriki katika mashindano makubwa manne, jambo ambalo limekuwa miongoni mwa heshima kubwa zaidi maishani mwangu.”

Matarajio kwa Timu ya Taifa ya England

Trippier aliongeza kuwa ana imani kubwa kuwa kikosi cha England kilichopo sasa kitafanikiwa kushinda mashindano makubwa siku za usoni. Alitoa shukrani kwa wachezaji wenzake kwa muda wote waliocheza pamoja na kufikia mafanikio makubwa kama kufika fainali mbili za Euro na nusu fainali ya Kombe la Dunia.

Trippier pia aliwapongeza mashabiki wa England kwa sapoti yao ya dhati, wakisafiri dunia nzima kuisapoti timu hiyo hata katika nyakati ngumu. “Naomba niwatakie Lee Carsley, benchi lake la ufundi, na timu kwa ujumla kila la heri kwa mustakabali wa timu ya taifa ya England,” alihitimisha Trippier.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba Mechi za Barcelona UEFA 2024/2025
  2. Ratiba Mechi za Real Madrid UEFA 2024/2025
  3. Ratiba Mechi za Liverpool UEFA 2024/2025
  4. Droo ya Ligi ya Mabingwa UEFA 2024/2025
  5. Matokeo Kagera Sugar Vs Yanga Leo 29/08/2024
  6. Matokeo KMC vs Coastal Union Leo 29/08/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo