Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024 2025

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup

Baada ya mechi kali za hatua ya 16 bora, timu nane zimefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB Tanzania kwa msimu wa 2024/2025. Mashindano haya yameendelea kushika kasi huku timu mbalimbali zikionesha ushindani mkubwa katika mbio za kutwaa ubingwa wa mashindano haya yanayoheshimika nchini.

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025

Safari ya Timu Zilizofuzu

JKT Tanzania imekuwa miongoni mwa timu zilizofanikiwa kutinga robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya Kwanza. Ushindi huu umeifanya JKT Tanzania kuwa moja ya timu zinazowania taji kwa nguvu mpya msimu huu.

Singida Black Stars nayo imefanikiwa kufuzu baada ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya KMC. Mbeya City ilijihakikishia nafasi kwenye robo fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, huku ikionesha ubora mkubwa wa safu yake ya ushambuliaji.

Stand United imeandika historia kwa kufuzu hatua hii muhimu kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Giraffe Academy, ushindi uliowaweka katika orodha ya timu zinazowania taji la Kombe la Shirikisho la CRDB Tanzania.

Timu zingine zilizofuzu robo fainali ni mabingwa watetezi Yanga SC, watani wao Simba SC, pamoja na Kagera Sugar na Pamba Jiji FC, ambazo zimeonyesha uwezo wa hali ya juu katika michuano hii.

Orodha Kamili ya Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025

  1. JKT Tanzania
  2. Mbeya City
  3. Singida Black Stars
  4. Stand United
  5. Simba SC
  6. Kagera Sugar
  7. Yanga SC
  8. Pamba Jiji FC

Mashabiki wa soka nchini wanatarajia kuona mechi za robo fainali zilizojaa ushindani mkubwa, huku kila timu ikipambana kwa lengo la kutwaa ubingwa wa CRDB Federation Cup kwa msimu wa 2024/2025. Michuano inaendelea kushika kasi, na hakika mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona timu gani itaibuka kidedea na kutinga hatua ya nusu fainali.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025
  2. Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025 Saa Ngapi?
  3. Hispania, Morocco na Ureno Wataka Kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake 2035
  4. Aishi Manula Bado Mambo Magumu Msimbazi
  5. Kane Atazamia Kufikia Rekodi ya Shilton na Kuweka Historia Mpya Uingereza
  6. Yaliyojiri Mkutano wa Waziri Kabudi na TFF, TPLB, Yanga na Simba
  7. CAF Yaondoa Marufuku Uwanja wa Benjamin Mkapa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo