Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe La Shirikisho Afrika 2024/2025

Thamani ya Kombe La Shirikisho Afrika CAF Confederation Cup

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe La Shirikisho Afrika 2024/2025 | Timu Zilizofuzu Robo Fainali CAF Confederation Cup: Michezo ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika inakaribia kufikia tamati huku vilabu vikubwa barani Afrika vikihangaika kuwania nafasi za kufuzu kwa hatua ya robo fainali. Tayari baadhi ya timu zimejihakikishia nafasi ya kusonga mbele, huku zingine zikitegemea mechi za mwisho ili kuamua hatima yao. Msimu huu wa 2024/2025 mashindano ya shirikisho yameonyesha ushindani mkubwa, lakini pia umetupa mabingwa wapya wanaochipukia katika mashindano haya.

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe La Shirikisho Afrika 2024/2025

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe La Shirikisho Afrika 2024/2025

  1. Zamalek
  2. RS Berkane
  3. Stellenbosch
  4. USM Alger
  5. Simba SC
  6. CS Constantine

Zamalek

Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho, Zamalek SC, walihitimisha safari yao ya hatua ya makundi kwa ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Black Bulls ya Msumbiji. Timu hiyo ya Misri, ikiwa haijapoteza mchezo wowote, sasa inaongoza Kundi D ikiwa na alama 11 na imefuzu huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Mshambuliaji Hossam Ashraf alikuwa nyota wa mchezo huo, akifunga mabao mawili ndani ya dakika mbili za kipindi cha pili. Bao la kwanza lilipatikana dakika ya 51 kupitia mpira uliorudi kwake baada ya krosi iliyozuiwa vibaya na walinzi wa Black Bulls.

Dakika mbili baadaye, aliongeza bao la pili kwa kumalizia mpira kwa ustadi mkubwa. Ingawa Black Bulls walijibu kupitia kichwa safi cha Egaita Efone dakika ya 62, bao la Ahmed Sayed Zizo dakika ya 83 lilihakikisha ushindi wa Zamalek na kuizika kabisa Black Bulls, ambao sasa wapo mkiani mwa kundi hilo na alama nne pekee.

Stellenbosch Yaandika Historia Dhidi ya Stade Malien

Klabu ya Stellenbosch kutoka Afrika Kusini imejiunga rasmi na hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stade Malien. Ushindi huu uliwapa nafasi ya pili kwenye Kundi D, wakiwa nyuma ya Renaissance Berkane ya Morocco.

Fawaz Basadin alifungua ukurasa wa mabao kwa penalti safi dakika ya 30, kabla ya Jayden Adams kuongeza bao la pili dakika tisa baadaye kwa mpira wa kichwa uliojaa ufundi. Stellenbosch walitawala mchezo huo na sasa wana alama tisa, huku Stade Malien wakibakia na alama nne na kufuzu kwao kuwa ndoto.

Berkane Yathibitisha Ubabe wa Kundi B

Renaissance Berkane, mabingwa wa zamani wa Kombe la Shirikisho, walihakikisha uongozi wao wa Kundi B baada ya sare tasa ya 0-0 dhidi ya Luanda Sol ya Angola. Licha ya kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake muhimu, Berkane walionyesha uwezo wa juu kwa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

Wakiwa na alama 13, Berkane wako kileleni mwa kundi wakiwa mbele ya Stellenbosch kwa alama nne. Luanda Sol, kwa upande mwingine, wanashika mkia wakiwa na alama mbili pekee, huku safari yao kwenye mashindano haya ikifikia ukingoni.

USM Alger Yatamba Dhidi ya Orapa United na Kufuzu

USM Alger ya Algeria nayo haikuachwa nyuma, baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Orapa United ya Botswana. Sekou Gassama aliwaweka wageni kifua mbele dakika ya 14, na Hossam Ghosha akaongeza bao la pili dakika ya 60. Ingawa Kamogelo Moloi aliwapa wenyeji bao la kufutia machozi dakika za mwisho, haikutosha kuizuia USM Alger kufuzu.

Kwa ushindi huu, USM Alger wanaongoza Kundi 3 wakiwa na alama 11, na wamejihakikishia nafasi ya robo fainali kabla ya mechi yao ya mwisho. Orapa United wameshindwa kupata ushindi wowote, wakibaki mkiani na alama mbili.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
  2. Kikosi cha Yanga VS Al Hilal Leo 12/01/2025
  3. Matokeo ya Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025
  4. Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
  5. Matokeo ya Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025
  6. Kikosi cha Simba VS Bravos do Maquis Leo 12/01/2025
  7. Ratiba ya Mechi za Leo 12/01/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo