Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025

Timu Zilizofuzo Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025 | Timu Zilizofuzu Hatua ya Robo Fainali CAF Champions

Michezo ya hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Afrika inakaribia kufikia tamati huku vilabu mbalimbali vikihangaika kuwania nafasi za kufuzu kwa hatua ya robo fainali. Tayari baadhi ya timu zimejihakikishia nafasi ya kusonga mbele, huku zingine zikisubiri mechi za mwisho kuamua hatima yao. Hadi sasa, Al Hilal ya Sudan ndiyo timu pekee iliyojihakikishia tiketi ya robo fainali, huku timu nyingine zikisalia kupambana katika mzunguko wa mwisho wa makundi.

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025

  1. Al Hilal Omdurman
  2. ASFAR
  3. Pyramids Fc
  4. Orlando Pirates
  5. Al Ahly

Al Hilal Omdurman

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025

Al Hilal Omdurman, moja ya vigogo wa soka Sudan, ndio klabu ya kwanza kujipatia tiketi ya hatua ya robo fainali ikiwa na alama 10 huku ikiwa kileleni mwa kundi A. Timu hii inatarajia kukamilisha hatua ya makundi kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Young Africans ya Tanzania mnamo Januari 12. Young Africans, baada ya ushindi wa kuridhisha dhidi ya TP Mazembe katika mechi iliyopita, wanahitaji matokeo mazuri kuhakikisha nafasi yao katika hatua ya robo fainali. Wakati huo huo, MC Alger itaikaribisha TP Mazembe mnamo Januari 10, ambapo ushindi kwa wenyeji utawakaribisha karibu zaidi na tiketi ya robo fainali.

Ratiba ya Mechi za Mzunguko wa Mwisho

Kundi A

  • MC Alger vs TP Mazembe – 10 Januari, 19:00 GMT
  • Al Hilal Omdurman vs Young Africans – 12 Januari, 19:00 GMT

Kundi B

  • Maniema Union vs Mamelodi Sundowns – 11 Januari, 13:00 GMT
  • FAR Rabat vs Raja Casablanca – 11 Januari, 19:00 GMT

Kundi C

  • Stade d’Abidjan vs Al Ahly – 11 Januari, 16:00 GMT
  • Orlando Pirates vs CR Belouizdad – 12 Januari, 13:00 GMT

Kundi D

  • Sagrada Esperança vs Pyramids – 11 Januari, 16:00 GMT
  • Djoliba vs Esperance – 12 Januari, 16:00 GMT

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Rachid Taoussi Apania Kushusha Nyota Zaidi Dirisha Dogo
  2. AS Vita Yamnyakua Dennis Modzaka Kutoka Coastal Union
  3. Rabbin Sanga Ajiunga na Tanzania Prisons Kwa Mkopo
  4. Robert Matano Ateuliwa Kuwa Kocha Mkuu wa Fountain Gate FC
  5. Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
  6. Mazembe Yaondolewa Ligi ya Mabingwa na MC Alger Baada ya Kipigo cha 1-0
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo