Tarehe Ya Kuripoti Shule Kidato Cha Tano 2024

Tarehe Ya Kuripoti Shule Kidato Cha Tano 2024

Tarehe Ya Kuripoti Shule Kidato Cha Tano 2024 | Ratiba ya Kuripoti Shule Wanafunzi wa Kidato cha Tano Mwaka 2024

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza tarehe rasmi za kuripoti kwa wanafunzi waliofanikiwa kupata nafasi za kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka wa masomo 2024.

Mwaka huu, jumla ya watahiniwa 572,359 walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne, ambapo 37.42% walifaulu kwa kupata daraja la I mpaka III hali inayoonesha kuwa ufaulu wa watahiniwa wa mwaka 2023 umeongezeka kwa 0.47% ikilinganishwa na ufaulu wa Daraja la I – III wa watahiniwa 192,348 (36.95%) wa mwaka 2022. Kati ya waliofaulu, wanafunzi 188,787 wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 812, wamepata nafasi za kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali nchini na vyuo vya ufundi.

Zoezi hili la uchaguzi limezingatia sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014, pamoja na mtaala ulioboreshwa. Lengo kuu la serikali ni kuhakikisha kila mwanafunzi mwenye sifa anapata nafasi ya kuendelea na masomo yake, hasa katika kipindi hiki ambapo elimu inatolewa bila malipo.

Tarehe Ya Kuripoti Shule Kidato Cha Tano 2024

Tarehe Ya Kuripoti Shule Kidato Cha Tano 2024

Shule za Sekondari: Wanafunzi wa kidato cha tano wanatakiwa kuanza kuripoti shuleni kuanzia tarehe 30 Juni, 2024. Siku ya mwisho ya kuripoti itakuwa tarehe 14 Julai, 2024. Muhula wa kwanza wa masomo ya kidato cha tano utaanza rasmi tarehe 1 Julai, 2024.

Vyuo vya Ufundi: Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi watapokea maelekezo ya kuripoti moja kwa moja kutoka kwenye vyuo husika.

Taarifa Zaidi Kuhusu Majina ya Waliochaguliwa Kidato Cha Tano 2024

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa na fomu za kujiunga zinapatikana kwenye tovuti za:

  • Ofisi ya Rais – TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET): www.nactvet.go.tz

Pia unaweza kutazama orodha ya majina ya wanafunzi waliopangiwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya kati kupitia viungo vilivyopo kwenye jedwali apa chini. Bofya jina la mkoa ambapo ulihitimu masomo ya sekondari ili kuangalia shule uliyo pangiwa.

ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA
GEITA IRINGA KAGERA
KATAVI KIGOMA KILIMANJARO
LINDI MANYARA MARA
MBEYA MOROGORO MTWARA
MWANZA NJOMBE PWANI
RUKWA RUVUMA SHINYANGA
SIMIYU SINGIDA SONGWE
TABORA TANGA

Kwa maswali au maelezo zaidi, wazazi/walezi na wanafunzi wanaweza kutembelea ofisi za elimu za mikoa na halmashauri au kupiga simu kwa namba za Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI: 026 160210 au 0735 160210.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tarehe ya Kuripoti Kambini JKT Mujibu wa Sheria 2024
  2. Sikukuu za Kitaifa Tanzania 2024
  3. Jinsi ya Kujiunga na JKT (Jeshi La Kujenga Taifa)
  4. Orodha ya Shule Nzuri za Advanced za Serikali Tanzania
  5. Sifa za Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo