Taoussi Huenda Akawa Kocha Mpya wa Azam FC, Mazungumzo Yanaendelea

Taoussi Huenda Akawa Kocha Mpya wa Azam FC Mazungumzo Yanaendelea

Taoussi Huenda Akawa Kocha Mpya wa Azam FC, Mazungumzo Yanaendelea

Azam FC, baada ya kumtimua kocha wao Yousouf Dabo kutokana na matokeo yasiyoridhisha, wapo kwenye harakati za kumpata kocha mpya. Kwa mujibu wa taarifa za ndani, kocha Rachid Taoussi, raia wa Morocco, ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kupewa mikoba hiyo.

Taoussi, mwenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika, amewahi kuzifundisha timu kadhaa za Morocco ikiwemo RS Berkane, FAR Rabat, Raja Casablanca, Olympique Club de Khouribga na Wydad Casablanca. Pia amewahi kuhudumu kama kocha wa timu ya taifa ya Morocco chini ya miaka 17, 20 na 23.

Taoussi Huenda Akawa Kocha Mpya wa Azam FC, Mazungumzo Yanaendelea

Chanzo cha ndani kutoka Azam FC kimethibitisha kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanaendelea vizuri.

“Kila kitu kinaenda vizuri hadi sasa katika mchakato wa kumpata kocha mpya ingawa hatutaki kufanya maamuzi ya haraka kwa sababu tunahitaji kupata mtu sahihi atakayeleta mabadiliko ya kiuchezaji kikosini,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, ametoa taarifa rasmi akisema kuwa kwa sasa timu itaendelea kufundishwa na makocha wa timu za vijana chini ya Kassim Liogope na Mohamed Rijkaard hadi hapo kocha mpya atakapopatikana.

Kuteuliwa kwa Taoussi kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika kikosi cha Azam FC ambacho kimekuwa kikisuasua katika michezo ya hivi karibuni. Mashabiki wa Azam FC wanasubiri kwa hamu kuona kama Taoussi ndiye atakayekuwa kocha wao mpya na kama ataweza kuirudisha timu kwenye ubora wake.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mbeya City FC Kucheza Dhidi ya Real Nakonde Siku ya Mbeya City Day
  2. Simba na JKT Tanzania Kuvaana Katika Mechi ya Kirafiki 07 Septemba
  3. Yanga Kumenyana na Cosmopolitan Katika Mechi ya Kirafiki KMC Complex
  4. Nassor Saadun Hamoud Asaini Mkataba Mpya na Azam FC
  5. Clement Mzize: “Nina Hatari Zaidi Nikitokea Benchi”
  6. Messi na Ronaldo nje Ballon d’Or 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo