Tanzania yatinga AFCON 2025 Kibabe

Tanzania yatinga AFCON 2025 Kibabe

Tanzania yatinga AFCON 2025 Kibabe

Dar es Salaam. Taifa Stars imefanikiwa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kwa kishindo kikubwa baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Guinea katika mechi ya mwisho ya kundi H. Ushindi huo, uliopatikana Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, umewaweka Tanzania katika nafasi ya pili kwenye kundi lao, nyuma ya DR Congo, na kuwafanya waibuke washindi kibabe wakijihakikishia nafasi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa mara ya nne.

Tanzania yatinga AFCON 2025 Kibabe

Safari ya Taifa Stars Kuelekea Morocco

Tanzania imekuwa na historia ya kuvutia katika kufuzu michuano ya AFCON, na ushindi huu wa kihistoria umeifanya Stars kujihakikishia tiketi ya kushiriki AFCON 2025 nchini Morocco. Hii ni mara ya nne kwa Taifa Stars kufuzu, ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1980 nchini Nigeria, ikafuatiwa na 2019 nchini Misri, kisha 2023 Ivory Coast, na sasa 2025 Morocco.

Katika hatua ya makundi, Stars ilipambana vilivyo kuhakikisha inaibuka nafasi ya pili nyuma ya DR Congo, huku Guinea ikiishia nafasi ya tatu na Ethiopia ikiburuza mkia.

Simon Msuva Aendelea Kung’ara

Bao pekee la ushindi kwa Tanzania lilifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 61, akiunganisha krosi maridadi kutoka kwa Mudathir Yahya. Bao hili liliwapa mashabiki wa Tanzania sababu ya kusherehekea kwa furaha kubwa.

Kwa mara nyingine tena, Msuva ameonyesha uwezo wake wa kufunga mabao muhimu, ikiwa ni kumbukumbu ya mchango wake mwaka 2019 aliposaidia Stars kufuzu kwa AFCON kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Uganda.

Ulinzi Imara Dhidi ya Sehrou Guirassy

Mshambuliaji hatari wa Guinea, Sehrou Guirassy, aliyekuwa kinara wa ufungaji katika mechi za kufuzu, alizimwa kabisa na mabeki wa Taifa Stars, Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ na Dickson Job. Wawili hao walihakikisha Guirassy hapati nafasi yoyote ya kutishia lango la Stars, huku wakionyesha kiwango bora cha ulinzi.

Benchi la Ufundi Laonyesha Ubora: Kufuzu kwa Stars mwaka huu kunatawaliwa na historia mpya, kwani kwa mara ya kwanza, timu hiyo imeongozwa na kocha mzawa, Hemed Morocco. Huu ni ushindi wa kihistoria kwa benchi la ufundi la wazawa, likiwa na mafanikio makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa tangu mwaka 1980.

Zawadi za Rais na Mafanikio ya Kifedha: Taifa Stars imepokea zawadi ya TZS milioni 505 kufuatia kufuzu kwa michuano ya AFCON. Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, aliahidi zawadi hiyo kama motisha kwa wachezaji. Ahadi hizo zimekuwa chachu ya ushindi, huku Sh5 milioni zikitolewa kwa bao hilo pekee la ushindi.

Takwimu za Mechi: Tanzania Dhidi ya Guinea

Licha ya ushindi wa Stars, Guinea ilionekana kuwa na umiliki mkubwa wa mpira kwa asilimia 57.2 ikilinganishwa na Tanzania yenye asilimia 42.8. Hata hivyo, Stars walionyesha ukomavu kwa kushambulia mara 11, ikilinganishwa na mashuti matano ya Guinea.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Viingilio Mechi ya Simba SC vs FC Bravos do Maquis 27 Nov 2024
  2. Jezi Mpya za Yanga CAF 2024/2025
  3. Jezi Mpya ya Simba CAF 2024/2025
  4. Matokeo ya Tanzania vs Guinea leo 19/11/2024
  5. Kikosi cha Tanzania vs Guinea leo 19/11/2024
  6. Timu Zilizofuzu AFCON 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo