Tanzania Taifa Stars vs Congo Leo 15/10/2024 ni saa ngapi?

Tanzania Taifa Stars vs Congo Leo ni saa ngapi

Tanzania Taifa Stars vs Congo Leo 15/10/2024 ni saa ngapi?

Leo, tarehe 15 Oktoba 2024, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuwaka moto wakati Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, itakapovaana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo).

Mechi hii ya marudiano katika kampeni ya kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 imeanza kuamsha hisia kali miongoni mwa mashabiki wa soka, huku wengi wakijiuliza, je, Stars wataweza kulipiza kisasi cha kipigo cha bao 1-0 walichokipata ugenini?

Je Mechi ya Tanzania Taifa Stars vs Congo Leo Inaanza saa ngapi?

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, mechi hii inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Hii ni fursa muhimu kwa Taifa Stars kujipatia ushindi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika Kundi H. Ushindi wowote utawapandisha hadi pointi saba, huku sare ikiwaacha na pointi tano, bado wakiwa na matumaini ya kuwania nafasi ya pili.

Tanzania Taifa Stars vs Congo Leo 15/10/2024 ni saa ngapi?

Katika mchezo uliopita, Taifa Stars ilijitahidi kuonyesha kiwango bora ugenini licha ya kufungwa bao la kujifunga. Kocha Hemed Morocco amekiri kuona mapungufu katika safu ya ushambuliaji na utengenezaji wa nafasi, na anaamini kuwa kama mapungufu hayo yatatatuliwa, Stars ina uwezo wa kuibuka kidedea.

Hata hivyo, historia inaonyesha kuwa Taifa Stars imekuwa na rekodi mbaya inapocheza nyumbani. Wengi wanahusisha hili na presha kutoka kwa mashabiki ambao wamekuwa wakilaumu badala ya kuhamasisha. Tofauti na mashabiki wa nchi nyingine ambao huwa sehemu ya ushindi kwa timu zao, mashabiki wengi wa Tanzania huenda uwanjani “kuangalia mpira” na kukosoa badala ya kushangilia na kuwapa moyo wachezaji.

Je, leo itakuwa tofauti? Je, mashabiki watajitokeza kwa wingi na kuishangilia Taifa Stars mwanzo mwisho, bila kujali matokeo? Wadau wa soka nchini wanaamini kuwa kama mashabiki wataiga mfano wa wenzao wanaposhangilia Simba na Yanga, Taifa Stars inaweza kupata nguvu ya ziada na kuibuka na ushindi.

Mbali na hayo, wachezaji wa Taifa Stars wanapaswa kutambua umuhimu wa jezi ya taifa na kuingia uwanjani wakiwa na lengo moja tu – ushindi. Wanapaswa kucheza kwa kujituma na bila woga, wakijua kwamba wanawakilisha zaidi ya Watanzania milioni 60.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Man City na Liverpool Wapigania Saini ya Mchezaji wa Crystal Palace
  2. Ratiba ya NBC Championship Tanzania 2024/2025
  3. Guardiola Atoa Mapya Kuhusu Mustakabali Wake Man City
  4. Yanga Yataja Siri ya Ushindi Kwenye Dabi dhidi ya Simba
  5. Fountain Gate Yaahidi Ushindi Dhidi ya KMC Oktoba 20
  6. Che Malone Awataka Wachezaji wenzake Kua Makini Kwenye Mechi ya Watani Jumamosi
  7. Washindi wa Tuzo za Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025 Mwezi Septemba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo